TANGA.

Michuano ya Shimiwi inaendelea kushika kasi Jijini Tanga, ambako Timu ya mpira wa pete, kutoka Sekta ya Uchukuzi wamefanikiwa kuibuka naushindi wa goli 33-20 dhidi ya Wapinzani wake Wizara ya Maliasili na Utalii,Katika dimba la Polisi chumbageni, Mkoani Tanga.
Katika mchezo huo uliokuwa na upinzani mkali, Timu ya Uchukuzi ilifanikiwa kupata goli 19 kwa 7 katika kipindi cha kwanza na kwenye kipindi cha pili walifanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla ya magoli 33, kupitia kwa viungo wake makini Mary Kajigili na Zaituni Maige.

Kwa upande wa mchezo wa kuvuta kamba upande wa wanawake timu ya Sekta ya Uchukuzi iliwachapa 2-0 Timu ya Afya, na Sekta ya Ujenzi waliwashinda Wizara ya Mawasiliano kwa kuwavuta Roundi zote mbili 2-0, Huku Wizara ya Katiba na Sheria wakiichapa Ras Shinyanga kwa Mivuto
2-0.
Aidha Timu ya Wachezaji ya Wanaume katika upande wa Kuvuta Kamba Sekta ya Uchukuzi, imeibuka kidedea katika Roundi zote mbili kwa kuwachapa Tume ya Maadili 2-0.
Katika michezo mingine ya kuvuta kamba Ikulu waliwatoa suluhu ya bao 2- 0 Ras Dodoma, huku Wizara ya Ardhi wakipata pointi za bure baada ya Wakili mkuu wa serikali kutoonekane uwanjani, katika mchezo uliopigwa viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara.


Michuano Ya SHIMIWI Inatarajiwa kufikia Tamati Oktoba 14 ambapo Washindi watazawadiwa Zawadi Mbalimbali vikiwemo Vikombe.