TUFANYE KAZI KWA WELEDI KUMSAIDIA RAIS SAMIA – KAIRUKI.

OR-TAMISEMI.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Angellah Kairuki amewataka watumishi wote wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI kufanyakazi kwa weledi, utulivu na kwa ushIrikiano ili kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan

Akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI leo Oktoba 3, 2022 muda mchache baada ya kuapishwa katika Ikulu, jijini Dar-es-salaam, Waziri Kairuki amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa bidii huku wakidumisha ushirikiano na mshikamano kwa lengo la kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi

“Naomba msiniogope, tufanye kazi kwa ushirikiano kumsaidia Rais Samia ambaye ana imani kubwa na sisi, tutimize wajibu wetu, nipo tayari kufanya kazi na nyie, naombeni ushirikiano wenu,” amesema Kairuki.

Naye Naibu Waziri Ofisi ya Rais -TAMISEMI anayeshughulikia Elimu, Mhe. David Silinde amesema Serikali imewekeza fedha nyingi hasa kwenye sekta ya eimu na afya na kuwa wajibu wao ni kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha huduma kwa wananchi zinaimarika.

” Serikali imetoa fedha nyingi za kutekeleza miradi ya maendeleo kwenye sekta mbalimbali zikiwemo elimu na afya, hivyo tukiwa ni wasaidizi wa Mheshimiwa Rais Samia ni wajibu wetu kufanya kazi usiku na mchana, kuchapa kazi kwa bidii kuhakikisha Wizara inasonga mbele katika kuboresha na kuhudumia wananchi..

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *