
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), amehitimisha mafunzo ya wajasiriamali wanawake vijana yaliyoendeshwa na Taasisi ya Academy for Women Entrepreneurs (AWE) tawi la Mbeya yaliyofanyika leo Septemba 3, 2022 katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST).
Mafunzo hayo yanadhaminiwa na Ubalozi wa Marekani hapa nchini.



