DODOMA.

TAASISI ya Newface Creative imesema inatarajia kuwawezesha kiuchumi vijana wa kike 4000 waishio vijijini kupitia wa mradi mwanamke jasiri.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini hapa,Mwenyekiti wa Tasisi ya Newface Creative Abdul Jimson alisema mradi huo utaanzia katika wilaya ya Chamwino kwa kugawa taulo za kike na kutoa misaada kwa wazee wasio jiweza.
“Kwa Mkoa wa Dodoma tunatarajia kuwafikia vijana wasiopungua 4000 na tutaanzia wilaya ya Chamwino na Kongwa ambapo tutaweza kuwakimu mahitaji yao wanawake wenye uhitaji,”alisema
Aliongeza kuwa: “Lengo la kuelekeza mradi huu katika maeneo ya vijijini ni kutokana na kuonekana kuwa na changamoto nyingi zaidi kuliko mjini pia hawapewi kipaumbele wanaishi kama wakoloni.Tumewahi kufanya miradi mingine ikiwemo ugawaji wa madaftari kwa watoto yatima,mkuranga,Bagamoyo na Tuwangoma na kwa sasa tunarudisha nguvu kubwa Dodoma katika wilaya ya chamwino.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Newface Creative Alex Kapndila alikaribisha wadau kuwasaidia ili waweze kutatua changamoto za watanzania wengi ambao wanahitaji msaada.
Aliiomba serikali kuendelea kushirikiana na tasisi mbalimbali za kiraia katika kufikisha msaada kwa jamii.
“Unahitajika msaada kutoka kwa watu wakubwa ili tuweze kuwafikia wahitaji wengi na ukiangalia uhalisia nchini yetu ni kubwa na serikali haiwezi kuwafikia watu wote hivyo mashirika yanachukua nafasi hiyo,”alisema
Naye Katibu Tawala wa Newface Creative Barika Mwaisaka alisema katika kumuunga mkono Rais Samia kwani amekuwa akipambana katikakuhakikisha ndoto za wanachi zinafikiwa.
Alisema kupitia mradi wa mwanamke jasiri tunaahidi kufanikisha ndoto za wanawake wengi za kujikwamua kiuchumi.


