
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Alhaj Majid Mwanga ameibuka mshindi wa nafasi ya Kwanza akichaguliwa kuwa mjumbe wa mkutano mkuu CCM Taifa kutokea Wilaya hiyo .
Uchaguzi huo ulikua na wagombea 12(walio wania nafasi ya uwakirishi mkutano mkuu taifa), washindi watatu wa juu ndio wamepata nafasi hiyo,jumla ya kura 1562 zimepigwa Kati hizo 149 zimeharika huku Dc Majid Mwanga akiibuka kidedea kwa kupata kura 1202, akifuatiwa na Sabina Kinyowa kura 652 na Dkt. Chisuligwe Salum kura 543.
Baaada ya ushindi huo DC Mwanga amewashukuru wajumbe wa mkutano mkuu Wilaya kwa kumpa kura na kuahidi kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na viongozi wengine wa Chama na Serikali.

