
Imeelezwa kuwa, Kampuni ya Uchimbaji dhahabu ya Geita Gold Mining Limited ( GGML) inaongoza kwa kuwa kampuni ya uchimbaji madini nchini inayofanya vizuri katika kutimiza Wajibu wa Makampuni kwa Jamii (CSR).
Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko alipotembelea mgodi wa GGM ili kushuhudia miradi mipya ya uchimbaji dhahabu inayofanyika katika mgodi huo Mkoani Geita.

“Mimi ningependa tuwe wa kweli, nchi hii kampuni inayofanya vizuri kwenye CSR kwenye madini ya kwanza ni GGM. Wamefanya kazi nzuri,” amesisitiza Dkt. Biteko.
Ameongeza kuwa, kampuni hiyo imekuwa ikishirikiana na wananchi katika huduma mbalimbali kwa jamii zinazozunguka migodi hususan, katika ujenzi wa hospitali, shule, vifaa vya tiba ili jamii ipate huduma bora.
