
Wakazi wa Buguruni Kisiwani, Wilaya ya Ilala Mkoa wa Dar es salaa, wametuma Salamu maalum kwa Jeshi la Polisi kupitia kwa IGP. Camillius Wambura wakimtaka aendelee na Operesheni za kuwakabili Wahalifu hususani ni Panya Road, ambao wamekua wakihatarisha maisha yao.
Wananchi hao wamesema hayo wakati wa Mkutano wa Hadhara uliofanyika Shule ya Msingi GANA ambapo walitoa maoni yao kuhusiana na namna Jeshi la Polisi walivyojitoa kupambana na Panya Road na kutumia muda huo kutuma salamu maalum kwa IGP. Wambura.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa jiji la Dar es salaam Omari Kumbilamoto amewaambia sababu kubwa ya kuwepo PanyaRoad ni wazazi kuowasihi watoto wao kusoma licha ya jitihada zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kwenye utoaji wa Elimu Bure, hivyo amewataka kumuunga mkono Rais Samia kuitikia wito wake wa kuwapeleka shule.
