Michezo ya SHIMIWI Yapamba Moto Jijini Tanga

Na Mwandishi Wetu, Tanga

Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wiraza na Idara za Serikali na Mikoa (SHIMIWI) 2022, yanaendelea kupamba moto Oktoba 2, 2022 jijini Tanga kwa michezo mbalimbali kutimua vumbi ikiwemo mpira wa netiboli, mchezo wa kuvuta kamba kwa wanaume na wanawake na mpira wa miguu.

Mchezo wa Kamba ndiyo ulikuwa fungua dimba kwa mashindano hayo kwa sharamshamra huku timu zikivutana kwa kuonesha wamejiandaa ipasavyo na kuonesha umahiri wao.

Timu ya Idara ya Mahakama wanaume ndiyo ilikuwa ya kwanza kuanza mchezo huo katika viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara kwa kuwavuta timu ya Tume ya Haki za Binadamu kwa 2-0, Ofisi ya Rais Ikulu waliwavuta Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa 2-0 na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) waliwavuta Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa 2-0.

Timu nyingine za mchezo huo wanaume ni Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imepata ushindi wa 2-0 baada ya timu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kutoingia uwanjani, timu ya Bunge imewavuta Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara kwa 2-0 na timu ya Ofisi ya Waziri Mkuu Sera imewavuta timu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga kwa 1-0, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wamepata alama 2-0 naada ya timu ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kutokufika uwanjani na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi iewavuta timu ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa 2-0.

Kwa upande wa wanawake katika mchezo wa Kamba timu ya Idara ya Mahakama imewavuta timu ya Mkuu wa Mkoa wa Singida kwa 2-0, timu ya Wizara ya Maji imewavuta Wizara ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kwa 1-0, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imepata ushindi wa 2-0 baada ya timu ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kutofika uwanjani hapo na timu ya Wizara ya Kilimo imewavuta timu ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa 2-0.

Michezo mingine ya kuvuta Kamba kwa wanawake imewakutanisha timu za Wizara ya Mammbo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambao wamewavuta Bohari ya Dawa (MSD) kwa 2-0, timu ya Wizara ya Katiba na Sheria imewavuta Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa 2-0, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma imepata ushindi wa 2-0 baada ya timu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kutofika uwanjani.

Aidha, timu ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) wameivuta timu ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa 2-0, ya Ofisi ya Mkamu wa Rais imewavuta timu ya Ofisi ya Bunge kwa 2-0 timu ya Hazina wameivuta timu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwa 2-0, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) imewavuta Wizara ya Afya kwa 2-0, Wizara ya Madini wamepata ushindi wa 2-0 baada ya timu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutofika uwanjani na Wizara ya Mifugo na Uvuvi wameivuta timu ya Tume ya Haki za Binadamu kwa 2-0.

Mchezo mwingine ni mchezo wa Netiboli timu ya Ofisi ya Rais Ikulu imewafunga Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kwa 42-13; nayo Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo wamewafunga timu ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi kwa magoli 16-4; huku Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum wameifunga timu ya Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) kwa magoli 17-16; pia timu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ikijizolea magoli 40-0 baada ya timu ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kutofika uwanjani.

Wakati huo huo; timu za soka za Wizara ya Nishati na Ofisi ya Bunge leo zimeshindwa kufurukuta na kubanwa mbavu na wapinzani wao katika mchezo wa soka wa michuano ya Kombe la Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) iliyofanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari ya Popatlal.

Nishati walichapwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kwa magoli 5-1; huku Bunge walitoka sare na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ya bao 1-1.

Katika uwanja wa shule ya sekondari ya Usagara timu ya Wizara ya Katiba na Sheria walipata ushindi wa chee baada ya RAS Kigoma kuchelewa kufika uwanjani; nao Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma walipewa ushindi dhidi ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali baada kushindwa kufika uwanjani; nao Hazina waliwachabanga Maendeleo ya Jamii kwa magoli 5-0.

Kwa upande wa mchezo wa netiboli timu ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari waliwashinda Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa magoli 32-7 mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Polisi Chumbageni; huku timu ya Tue ya Taifa ya Ukaguzi waliwaliza Tume ya Utumishi wa Umma kwa magoli 24-7; na timu ya Hazina iliwachapa Bohari ya Dawa nchini (MSD) kwa magoli 33-7; nayo Wizara ya Madini walipata ushindi wa chee wa magoli 40 baada ya RAS Kilimanjaro walishindwa kufika uwanjani.

Katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Bandari timu ya Wizara ya Afya waliwafunga Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa magoli 31-23.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *