DKT. BITEKO ATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA MADINI NA TAASISI ZAKE KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA

Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adolf Ndunguru na Kamishna wa Madini Nchini, Dkt. Abdulrahman Mwanga leo tarehe 01 Oktoba, 2022 ametembelea Banda la Wizara ya Madini na Taasisi zake kwenye Maonesho ya Tano ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja Bombambili mjini Geita.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea maonesho, sambamba na kupongeza kwa maandalizi mazuri ameelekeza waoneshaji kuendelea kutoa elimu kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo kwenye Sekta ya Madini ili wananchi wengi waweze kushiriki na kunufaika

“Nitoe wito kuwa elimu hii iwe endelevu kwa wananchi kwa ujumla ili waweze kushiriki kikamilifu katika Sekta ya Madini,” amesisitiza Dkt. Biteko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *