WAZIRI AWESO AZINDUA BODI YA SITA YA WAKURUGENZI BONDE LA WAMI NA KUWEKA JIWE LA MSINGI.

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) Amezindua Bodi ya Sita ya Wakurugenzi Bonde la Wami/Ruvu na kuweka jiwe la Msingi la jengo la Ofisi Mpya za Bodi hiyo ambapo Hafla ya Uzinduzi huo imefanyika Mkoani Morogoro na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mkoa, kamati ya Siasa ya Mkoa, Kamati ya ulinzi na usalama, viongozi mbalimbali wa Dini, Menejimenti ya Bonde la Wami/ Ruvu Pamoja na Wadau mbalimbali wa Sekta ya Maji.

Katika Hafla hiyo Waziri Aweso ameitaka Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu kwenda kusimamia sheria ya usimamizi wa rasilimali za maji Kwa kuwashirikisha Wananchi kwa kuwapa elimu juu ya uhifadhi na utunzaji wa Vyanzo Vya Maji huku akibainisha kuwa Bonde la Wami/ Ruvu ndio liwe suluhisho la utatuzi wa changamoto za upatikani wa maji.

Aidha Waziri Aweso ametoa maagizo kwa mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Morogoro (Moruwasa) kuhakikisha anakamilisha mradi wa mguru wa ndege utakao wezesha upatikani wa maji safi kwa Wananchi waishio maeneo ya kihonda Mkoani Morogoro.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *