
Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ametoa ahadi ya kuchangia madawati 100 kupitia taasisi yake ya Tulia Trust kwa shule ya Msingi Ilomba iliyopo kata ya Isyesye Jijini humo mara baada ya kuelezwa changamoto ya uhaba wa madawati na wanafunzi wa shule hiyo wakati akiwa katika ziara zake za kikazi leo Septemba 30, 2022.
Wakati huohuo Dkt. Tulia amefanya halambee kwa baadhi ya Viongozi na Wananchi aliokuwa ameambatana nao katika ziara hiyo na kuwezesha kufanikisha ahadi ya upatikanaji wa jumla ya madawati 121.

