RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. SAMIA APOKEA MAELEZO KUTOKA KWA NAIBU KATIBU MKUU OFISI YA RAIS TAMISEMI.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea maelezo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Grace Magembe ya vifaa tiba Vipya ambavyo ni meza za upasuaji 79, taa za upasuaji 79, mashine za kutoa dawa za usingizi 10, mashine 82 za kidijitali za X-ray na seti ya samani 1,006 ya vitanda vya wagonjwa, magodoro na makabati ya vitanda vitakavyosambazwa kwenye vituo vya huduma za afya nchi.

Rais amepokea malezo hayo wakati akikagua mabanda katika hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Usimamizi wa shughuli za Lishe na tathmini ya Sita (6) ya Mkataba wa Lishe uliofanyika Ukumbi wa Jiji la Dodoma – Mtumba. Leo tarehe 30 Septemba 2022 (Picha na Eliud Rwechungura – OR TAMISEMI)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *