WANAMICHEZO RUDINI NA USHINDI: YAKUBU

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Bw. Saidi Yakubu amewaaga wanamichezo wa Wizara hiyo ambao wanakwenda kwenye Michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Wakala, Idara za Serikali na Mikoa (SHIMIWI) 2022 jijini Tanga.

Kaimu Katibu Mkuu Bw. Yakubu amewatakia wanamichezo hao safari njema na kuwahimiza kuwa Wizara hiyo ina imani nao kwenye mashindano hayo na kuwataka wawe mabalozi wazuri wakati wote wa mashindano hayo hatua itakayowafanya wacheze kwa kujituma na kurudi na ushindi.

Mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Octoba 1, 2022 jijini Tanga na yanatarajiwa kufunguliwa rasmi Oktoba 05, 2022 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na kuhitimishwa Oktoba 15, 2022.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *