WAHANGA WA UJAMBAZI WILAYANI SERENGETI, MKOANI MARA WATUMA SALAMU KWA IGP WAMBURA.

Leo Septemba 29, 2022 Wakazi wa Kijiji cha Nyamakobiti kilichopo Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara wametuma salamu za Pongezi na Ahsante kwa IGP Wambura na Jeshi lote la Polisi kwa Operesheni mbalimbali za kutokomeza wahalifu Kijijini hapo na maeneo mbalimbali nchini.

Wananchi hao wametuma salamu hizo kupitia mkutano wa hadhara wa wanakijiji ulioandaliwa na viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Nyamakobiti na maeneo ya jirani uliolenga kulipongeza jeshi la Polisi na kuliomba liendelee na operesheni hizo za kudhibiti wahalifu ili kijijini hapo paendelee kuwa sehemu salama na wananchi waweze kufanya shuguli za kujiletea maendeleo bila hofu yoyote.

Aidha, wahanga wa vitendo vya uhalifu katika kijiji hicho wametoa shuhuda mbalimbali kueleza namna walivyoteswa na matukio ya ujambazi kwa kuibiwa mali zao kama vile mifugo, pikipiki pamoja na kujeruhiwa na kuuliwa na Majambazi Sugu kijijini hapo kabla ya Jeshi la Polisi kuwashugulikia kikamilifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *