CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI WANAWAKE DODOMA WAKUTANA NA KATIBU WA NEC SHAKA HAMDU SHAKA.

Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Mkoa wa Dodoma (DWJ) jana Septemba 28,2022, kimekutana na kufanya mazungumzo na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Shaka Hamdu Shaka kwa dhamira ya kujitambulisha na kujadili namna ya kukijenga chama (DWJ) ili kuendelea kugusa jamii na kushirikiana na serikali.

Sekta ya elimu ni miongoni mwa sekta zinazotiliwa mkazo na DWJ kwa kuibua wanafunzi walioshindwa kuendelea na masomo kutokana na vikwazo mbalimbali ili wasaidiwe na kufikia ndoto zao kielimu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *