BASHUNGWA: “FUATILIENI MALALAMIKO YA POSHO ZA KUJIKIMU KWA WAAJIRIWA WAPYA”

Angela Msimbira OR –TAMISEMI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa amemuagiza Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia Elimu, Dkt. Charles Msonde kuhakikisha anafuatilia malalamiko ya waajiriwa wapya 9,800 kuhusu posho za kujikimu na viwango vya malipo vinavyotolewa.

Ametoa maagizo hayo Septemba 28, 2022 wakati akitoa taarifa kwa umma kuhusu maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza, januari, 2023, jijini Dodoma.

Bashungwa amesema kuwa amekuwa akipokea Malalamiko kutoka kwa baadhi ya watumishi wapya kuwa kuna baadhi ya Halmashauri bado hawajapewa posho za kujikimu na viwango vya posho vinatofautiana hali ambayo haikubaliki na kuagiza ufuatiliaji ufanyike ili kujiridhisha kuhusu malalamiko hayo.

β€œNimekuwa nikipokea malalamiko mengi kutoka kwa waajiriwa wapya 9,800 ambao wanakabiliana na changamoto ya kutokulipwa posho za kujikimu kwa wakati na viwango vya malipo vinatofautiana katika baadhi ya Halmashauri hili lifanyiwe kazi, ” amesema Bashungwa.

Amemuagiza Naibu Katibu Mkuu huyo kuhakikisha wanafanya uchambuzi wa kina kujua ni halmashauri gani ambazo hazijalipa posho kwa watumishi hao na viwango halisi vinavyotolewa.

Amesema baada uchambuzi huo na kushughulikia malalamiko hayo, ufafanuzi utolewe kwa waajiriwa hao ili kuwasaidia kutimiza majukumu yao kwa weledi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *