
Serikali imetoa shilingi bilioni Kumi na Tisa kwa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Mtwara (MTUWASA) ili kufumua mfumo wa usambazaji wa maji ambao ni chakavu na kuweka mpya.
Hatua hiyo itataua kero ya upatikanaji wa Maji kwa wakazi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani ambapo tayari Mamlaka hiyo imetiliana saini na Mkandarasi ili kuanza kutekeleza mradi huo.
Akishuhudia tukio la utiaji saini Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amemtaka mkandarasi anaekwenda kutekeleza mradi huo kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha unakamilika kwa wakati na kwa ubora, Aidha Mbunge wa Jimbo hilo ameishukuru sana Serikali na kuahidi kutoa ushirikiano juu ya ufatiliaji na usimamizi wa karibu wa Utekelezaji wa Mradi.


