MBULU WAMFURAHISHA BASHUNGWA UTEKELEZAJI WA MIRADI.

Na Angela Msimbira,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mji wa Mbulu kwa kusimamia kwa weledi miradi ya maendeleo inayotekelezwa na halmashauri hiyo.

Mhe. Bashungwa ametoa pongezi hizo leo Septemba, 27, 2022 wakati wa kukagua miradi ya maendeleleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Mji wa Mbulu mkoani Mayara.

Katika ziara hiyo, Mhe. Bashungwa alifungua madarasa mawili ya shule ya Sekondari Murray na jengo la maabara ya fizikia katika Shule ya Sekondari Hhaynu.

Amesema miradi hiyo imejengwa kwa viwango na thamani ya fedha iliyotumika imeenda sambamba na majengo yaliyojengwa.

Pia amekagua ujenzi wa bwalo katika shule ya Kainam High School na kituo cha afya cha Kaiman.

Aidha, Waziri Bashungwa ameziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa vituo vya afya viwe vimekamilika na kuanza kutoa hiduma kwa wananchi ifikapo Desemba 30, 2022

“ Ni dhamira ya Serikali kuhakikisha huduma bora za afya zinaboreshwa na zinasogezwa karibu wananchi, hivyo halmashauri zinatakiwa vituo vya afya vinavyojengwa katika maeneo yao vinakamilika na kuanza kutoa huduma.”

Waziri Bashungwa amekamilisha ziara yake ya kikazi katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu kwa kukagua miradi ya inayotekelezwa katika sekta za elimu, afya na ujenzi wa miundombinu ya barabara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *