WAZIRI MKENDA ATANGAZA UFADHILI KWA WANAFUNZI KUPITIA SAMIA SCHOLARSHIP.

Na; Deborah Munisi, Dodoma.


Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia imeanzisha Programu ya ufadhili iitwayo SAMIA SCHOLARSHIP kwa wahitimu wa kidato cha sita ambao utagaramia kwa asilimia miamoja kwa Wanafunzi ambao wamepata udahili katika fani za Teknolojia, masomo ya Sayansi, Uhandisi, na tiba ili kujiunga katika masomo ya Chuo Kikuu hapa nchini..
Akitangaza Juu ya Program hiyo Waziri wa Elimu, Sayansi, na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Ufadhili huu ni mpya hapa nchini kwa masomo ya Shahada ya kwanza kwa wanafunzi waliopata ufaulu wa juu katika mitihani ya Kidato cha Sita mwaka 2022 iliyoendeshwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) katika Tahasusi za Sayansi (PCB, PCM, PGM, CBG, CBA, PMC na CBN).

“Ufadhili huu ni mpya hapa nchini kwa masomo ya shahada ya kwanza kwa wanafunzi waliopata ufaulu wa juu katika mitihani ya Kidato cha Sita mwaka 2022 iliyoendeshwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) katika Tahasusi za Sayansi (PCB, PCM, PGM, CBG, CBA, PMC na CBN).”


Waziri Mkenda ametaja sifa za kupata Ufadhili huo kwa wahitimu wa kidato cha sita ikiwa ni kuwa na ufaulu wa juu kwenye mitihani ya Taifa ya kidato cha sita mwaka 2022 iliyoendeshwa na NECTA katika tasusi za Sayansi, na kuomba ufadhili kwa usahihi kwa njia iliyotolewa.

“Awe Mtanzania, Awe amepata udahili katika programu za Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, Hisabati au Tiba katika Chuo Kikuu hapa nchini kinachotambuliwa na Serikali ambazo zimetajwa katika kundi la kwanza (Cluster 1) katika Mwongozo wa utoaji mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mwaka 2022/2023 unaopatikana kupitia tovuti ya bodi ya mikopo Tanzania, Awe ameomba ufadhili kwa usahihi kwa njia iliyoelekezwa”

Amesema ufadhili huo utazingatia viwango na miongozo ya Bodi ya mikopo ya Elimu ya juu kwa kugaramia Malazi na Chakula,Ada ya mafunzo na Utafiti.
“Ufadhili utazingatia viwango na miongozo ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kugharamia maeneo yafuatayo: Ada ya Mafunzo, Posho ya chakula na malazi,Posho ya Vitabu na Viandikwa, Mahitaji Maalum ya Vitivo, Mafunzo kwa Vitendo,Utafiti, Vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu, na Bima ya Afya”

Aidha ametaja Masharti kwa mwanafunzi atakayepata ufadhili huo ikiwa ni sambamba na mnufaika kutoruhusiwa kuahirisha masomo, isipokuwa kwa sababu za kiafya, na kuthibitishwa na chuo husika.
“Mwanafunzi atakaepata ufadhili wa SAMIA SCHOLARSHIP atawajibika kuzingatia masharti yafuatayo:
Anapaswa kusoma, kuelewa na kusaini Mkataba wa Makubaliano ya Ufadhili wa Masomo kati yake na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia; Anapaswa kuwa na akaunti ya Benki kwa ajili ya fedha atakazolipwa moja kwa moja, Mnufaika hataruhusiwa kubadilisha programu ya masomo aliyopatia ufadhili bila barua ya idhini ya maandishi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mnufaika hataruhusiwa kuahirisha masomo, isipokuwa kwa sababu za kiafya, na kuthibitishwa na chuo husika, Ikiwa mnufaika ataghairi fursa ya ufadhili kabla ya kuanza masomo, atapaswa kuwasilisha taarifa ya maandishi
Ametangaza Orodha ya majina ya wanafunzi husika inapatikana kupitia www.moe.go.tz na Iwapo kiwango cha ufaulu wa mnufaika kitashuka chini ya GPA 3.8 katika mwaka wa masomo, ufadhili utasitishwa, Mnufaika anapaswa kujisajili katika Mfumo wa Usimamizi wa Wanafunzi (Students Management System) unaopatikana kupitia https://scholarships.moe.go.tz/www.heslb.go.tz kwa kuzingatia alama za ufaulu: 3-5 (ME), 3-6 (KE) na 5-9 (wenye mahitaji maalum).


Hata hivyo amesema ufadhili huo utawanufaisha wanafunzi 640, ukiwa na wasichana 244 sawa na asilimia 38, wavulanaa wakiwa ni 396 sawa na asilimia 62 huku kiwango cha wanafunzi wa alama tatu ni 60 sawa na asilimia 9.ambapo wanafunzi 11 sawa na asilimia 100 ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu waliopata daraja la kwanza katika tahasusi zilizolengwa.
Kuhusu muda wa fadhili amesema wanufaika watagaramiwa kati ya miaka mitatu hadi mitano kulingana na programu husika walizodahiliwa na kueleza utaratibu wa kuomba Ufadhili.
“Maombi ya Samia Scholarship yatawasilishwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa njia ya mtandao https://olas.heslb.go.tz kwa siku 14 kuanzia Septemba 28, 2022.”
Amehitimisha kwa kutaja shule zilizotia fora kwa idadi kubwa za wanufaika wa Samia Scholarship ikiwa ni Tabora Boys wanafunzi 79 (12%), St.Mary’s Mazinde Juu wanafunzi 51 (8%), Mzumbe Sekondari wanafunzi 46 (7%), Tabora Girls 39 (6%),Kisimili wanafunz`i 31 (5%)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *