WANANCHI TOENI USHIRIKIANO WA WATUMISHI – BASHUNGWA.

Angela Msimbira MANYARA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ametoa wito wananchi kutoa ushirikiano kwa watumishi wanaopangiwa kazi kwenye maeneo yao katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na Afya, Elimu na Utawala.

Akiongea na wananchi wa tarafa ya Hilbadaw, Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’ Mkoani Manyara amesema wananchi wanawajibu wa kushirikiana na watumishi ili kuleta maendeo kwa Halmashauri na Taifa kwa ujumla.

Bashungwa amesema Serikali inaleta watumishi wa umma kuchochea maendeleo hivyo tushirikiane nao katika kuhakikisha wanatimiza majukumu yao ikiwemo kuwapa huduma bora zinazoratibiwa na Serikali yao.

Amesema kuwa Serikali inawajibu wa kuwaletea maendeleo wananchi, hivyo kunahitajika ushirikiano na mshikamano kati ya wananchi na Serikali ikiwa ni pamoja na watumishi wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *