PROF.SHEMDOE ASHUKURU SERIKALI YA UINGEREZA KWA MSAADA WA MAGARI

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI) Prof. Riziki Shemdoe ameishukuru Serikali ya Uingereza kwa Msaada wa Magari mawili,ambayo nimuendelezo wa ushirikiano wa karibu wa serikali ya Tanzania na Uingereza.Ametoa shukrani hizo leo Septemba 26, 2022 wakati wa makabidhiano ya magari hayo katika Ofisi Ndogo ya TAMISEMI, Magogoni Jijini Dar-es-salaam.Amesema magari hayo yanaenda kusaidia kwenye maeneo ya Utawala bora na ukusanyaji wa mapato ya ndani ambavyo ni miongoni mwa vipaumbele vya Wizara.

Prof.Shemdoe ameiomba Serikali ya Uingereza kuendelea kuisaidia Wizara ya TAMISEMI pale wanapoona inafaa kuwasaidia na tayari wamekwisha waeleza vipaumbele vya Wizara hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *