1.0 UTANGULIZI
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeanzisha programu ya Ufadhili iitwayo SAMIA SCHOLARSHIP. Ufadhili huu ni mpya hapa nchini kwa masomo ya shahada ya kwanza kwa wanafunzi waliopata ufaulu wa juu katika mitihani ya Kidato cha Sita mwaka 2022 iliyoendeshwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) katika Tahasusi za Sayansi (PCB, PCM, PGM, CBG, CBA, PMC na CBN).
SAMIA SCHOLARSHIP itagharamia kwa asilimia mia moja (100%) masomo ya Chuo Kikuu kwa wanafunzi hao ambao wamepata udahili katika fani za Teknolojia, Uhandisi, Hisabati na Tiba.
2.0 SIFA ZA KUPATA UFADHILI
Ufadhili huu utatolewa kwa wahitimu wa kidato cha sita wenye sifa zifuatazo:
2.0 SIFA ZA KUPATA UFADHILI
Ufadhili huu utatolewa kwa wahitimu wa kidato cha sita wenye sifa zifuatazo:
i. Awe Mtanzania;
ii. Awe na ufaulu wa juu kwenye mitihani ya taifa ya kidato cha sita mwaka 2022 iliyoendeshwa na NECTA katika tahasusi za sayansi;
iii. Awe amepata udahili katika programu za Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, Hisabati au Tiba katika Chuo Kikuu hapa nchini kinachotambuliwa na Serikali ambazo zimetajwa katika kundi la kwanza (Cluster 1) katika Mwongozo wa utoaji mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mwaka 2022/2023 unaopatikana kupitia iii. www.heslb.go,tz
iv. Awe ameomba ufadhili kwa usahihi kwa njia iliyoelekezwa;
Awe Mtanzania;
i. Awe na ufaulu wa juu kwenye mitihani ya taifa ya kidato cha sita mwaka 2022 iliyoendeshwa na NECTA katika tahasusi za sayansi;
ii. Awe amepata udahili katika programu za Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, Hisabati au Tiba katika Chuo Kikuu hapa nchini kinachotambuliwa na Serikali ambazo zimetajwa katika kundi la kwanza (Cluster 1) katika Mwongozo wa utoaji mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mwaka 2022/2023 unaopatikana kupitia ii. www.heslb.go,tz
iii. Awe ameomba ufadhili kwa usahihi kwa njia iliyoelekezwa;
Ufadhili utazingatia viwango na miongozo ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kugharamia maeneo yafuatayo:
(a) Ada ya Mafunzo
(b) Posho ya chakula na malazi
(c) Posho ya Vitabu na Viandikwa
(d) Mahitaji Maalum ya Vitivo
(e) Mafunzo kwa Vitendo
(f) Utafiti
(g) Vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu
(h) Bima ya Afya
2.0 MUDA WA UFADHILI
Wanafunzi watakaofadhiliwa, watagharamiwa kati ya miaka mitatu (03) hadi mitano (05) kulingana na programu husika walizodahiliwa.
2.0 UTARATIBU WA KUOMBA UFADHILI
Maombi ya Samia Scholarship yatawasilishwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa njia ya mtandao https://olas.heslb.go.tz kwa siku 14 kuanzia Septemba 28, 2022.
3.0 WAJIBU/MASHARTI YA UFADHILI
Mwanafunzi atakaepata ufadhili wa SAMIA SCHOLARSHIP atawajibika kuzingatia masharti yafuatayo:
(a) Anapaswa kusoma, kuelewa na kusaini Mkataba wa Makubaliano ya Ufadhili wa Masomo kati yake na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia;
(b) Anapaswa kuwa na akaunti ya Benki kwa ajili ya fedha atakazolipwa moja kwa moja.
(c) Mnufaika hataruhusiwa kubadilisha programu ya masomo aliyopatia ufadhili bila barua ya idhini ya maandishi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia;
(a) Mnufaika hataruhusiwa kuahirisha masomo, isipokuwa kwa sababu za kiafya, na kuthibitishwa na chuo husika;
(b) Ikiwa mnufaika ataghairi fursa ya ufadhili kabla ya kuanza masomo, atapaswa kuwasilisha taarifa ya maandishi kwenda kwa:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,
Mji wa Serikali Eneo la Mtumba Mtaa wa Afya,
S.L.P 10,
40479 DODOMA, TANZANIA.
Barua pepe: ps@moe.go.tz
(c) Iwapo kiwango cha ufaulu wa mnufaika kitashuka chini ya GPA 3.8 katika mwaka wa masomo, ufadhili utasitishwa;
(d) Mnufaika anapaswa kujisajili katika Mfumo wa Usimamizi wa Wanafunzi (Students Management System) unaopatikana kupitia https://scholarships.moe.go.tz/
MUHIMU KUZINGATIA:
(a) Ufadhili huu ni wa asilimia mia moja ambao kikomo chake kitazingatia miongozo ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.
(b) Orodha ya majina ya wanafunzi husika inapatikana kupitia (b) www.moe.go.tz na (b) www.heslb.go.tz
(c) Alama za ufaulu: 3-5 (ME), 3-6 (KE) na 5-9 (wenye mahitaji maalum)
UCHAMBUZI WA WANUFAIKA 640 wa SAMIA SCHOLARSHIP
⦁ Uwiano wa kijinsia wa wanufaika 640 wa Samia Scholarship ni; Wasichana 244 na asilimia 38% na Wavulana ni 396 sawa na asilimia 62%.
⦁ Wanafunzi kutoka shule za serikali ni 396 sawa na asilimia 62% wakati Wanafunzi kutoka shule za binafsi ni 244 sawa na asilimia 38%.
⦁ Wanafunzi wenye ufaulu wa juu kiwango cha Alama tatu (3) ni 60 (9%)
⦁ Wanafunzi kutoka shule za Tanzania Visiwani ni 43 (7%)
⦁ Wanafunzi kutoka shule za Tanzania Bara 597 (93%)
⦁ Aidha jumla ya wanafunzi 11 wenye mahitaji maalumu watanufaika na Samia Scholarship. Hawa ni asilimia 100 ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu waliopata darala la kwanza katika tahsusi zinazolengwa na Samia Scholarship mwaka 2022/23
⦁ Shule zilizotia fora kwa kuwa na idadi kubwa za wanufaika wa Samia Scholarship ni pamoja na:
i. Tabora Boys wanafunzi 79 (12%)
ii. St.Mary’s Mazinde Juu wanafunzi 51 (8%)
iii. Mzumbe Sekondari wanafunzi 46 (7%)
iv. Tabora Girls 39 (6%)
v. Kisimili wanafunzi 31 (5%)