Na Deborah Munisi: Dodoma.

Imebainishwa kuwa uboreshwajiwaji wa Sera na Rasimu ya Mitaala ya Elimu hapa nchini inaweza kuwa chachu ya maendeleo kwa wanafunzi kunufaika kupata elimu ujuzi kwa mustakabali wa Taifa.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda wakati akifungua Mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wa Elimu wa Tanzania Bara na Visiwani unaoendelea Jijini Dodoma hadi Septemba 28 Mwaka huu.
“Tumeshapokea maoni mengi sana na tunaendelea kupokea, wadau wachukue sera ya elimu ya mwaka 2014 waone nini kibaki vile vile na ninini kiongezwe nini kibadilishwe kama mabadiliko ni makubwa sana lazima tuanze na sera mpya na kama mabadiliko ni kidogo na ya msingi basi tunatoa toleo jipya la sera ambalo linaunganisha yale yote tuyotaka kuyaongezea” Alisema Waziri Mkenda.
Mkenda amesema, kwa sasa kuna umuhimun wa kufanya mabadiliko ya sera na mitaala ili kuhakikisha elimu yetu inakuwa bora na kuleta ujuzi.
“Sasa hivi mtu hazungumzii tu elimu bila kufanya mageuzi, Nchi yetu ilikubali kusaini Sastainable Development Goals kwa hiari yetu yapo mambo ambayo lazima tukubali kuyafanya na mengine tuaendelea kuyatekeleza, Wakati tunapitia Mitaala tunataka na sisi kuendana na Dunia na Suala la Mageuzi ya Elimu siyo ya Tanzania peke yake.”

Amesema, maboresho katika sekta ya elimu hapa nchini ni kufuatia kauli ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe Samia Suluhu Hassan
“Elimu Ujuzi ni ile ambayo itampa mtoto mwelekeo kutoka kidato cha nne na kubahatika kwenda kidato cha tano na cha sita, angalau anajua nielekee wapi? kuna nini? na ntakwenda kufanya nini? kwahiyo ndo maana sasa tunabadilisha mitaala wa elimu Tanzania.”
Ameongeza kuwa, Suala la Mitaala ni la Kiufundi, hivyo wanatumaini maoni kupitia maoni hayo ya wadau yatafanya Mageuzi katika Sekta ya Elimu, na hiyo itasaidia kufanya maamuzi Thabiti sambamba na Lugha ya kufundishia na kisishushe viwango vya elimu.
Mkutano huo umeambatana na kikao cha ndani chenye lengo la wadau wa elimu kupitia sera na mitaala ya Elimu hapa nchini.

Kwa Upande wao Baadhi ya wadau wa elimu waliohudhuria katika mkutano huo wametoa maoni yao akiwemo Mdhibiti Mkuu Ubora Wa Shule Kanda ya Magharibi Bi. Edith Mwaijage yeye amesema ipo haja ya maboresho ya sera ya mitaala ili kuondoa hali ya sintofahamu kwa baadhi ya wadau wa Elimu na wasio wa elimu, kwa mfano umri wa mwanafunzi kujiunga shule na kuhitimu.
“Kuna mambo ambvayo yalionekana yanaleta ukakasi, licha ya wengine walielewa lakini wengine hawakuielewa kwa mfano umri wa mwanafunzi au muda wa wanafunzi kupata elimu ya msingi hadi elimu ya juu”

Naye Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Elimu ya Zanzibar Abdallah Musa amesema suala la elimu katika nchi yoyote lazima huzingatia sera na mitaala husika hivyo sera ya elimu ina dira kubwa kwa mwanafunzi wa Tanzania Bara na Visiwani.
“Ingawa Mabadiliko tunayoenda nayo sasa ya Sayansi na Teknolojia bado inatakiwa tuendelee kuimarisha sera zetu hasa tukizingatia mtoto akimaliza elimu ya lazima aonyeshe viashiria vya kuweza kujitegemea, tuangalie baada ya muda wa kumaliza elim u ya msingi je? mwanafunzi ametoka na ujuzi gani.”
