SILAHA NYINGINE YASALIMISHWA MORO(JOSEPHINE ASALIMISHA SILAHA).

Mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la JOSEPHINE MAGANGA mwenye umri wa miaka 62 mkazi wa mtaa wa Mzigila kata ya Boma manispaa ya Morogoro amekabidhi silaha kwa jeshi la Polisi leo tarehe 24.09.2022,

Akiongea na afisa mnadhimu namba 1 wa Polisi Mkoa wa Morogoro ACP HASSAN MAYA wakati anamkabidhi, mama huyu amesema silaha hiyo sina ya GOBOLE ilikuwa inatumiwa na marehemu mume wake aliekuwa afisa wa Maliasili.

“Hapo mwanzo nilikuwa naogopa kuisalimisha lakini baada ya askari wa kata yetu ya boma kufanya kikao na sisi nakunitoa wasiwasi juu ya usalama wangu, nikaona niisalimishe” ameongea mama huyo.

ACP HASSAN MAYA alimpongeza mama huyo kwa kufikia maamuzi hayo na kuwaasa wa kazi wa mtaa huo kama kuna mwengine anasilaha asiogope kusalimisha kwani kipindi hichi cha kuanzia tarehe 01.09 hadi 31.10.2022 ni kipindi cha Usalimishaji silaha kwa hiari na ukifanya hivyo hautachukuliwa hatua yoyote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *