MKURUGENZI AWATAKA WAALIMU KUANZISHA KIKUNDI CHA AKIBA NA MIKOPO (SACCOS).

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Sunday Deogratias amewataka walimu kuanzisha kikundi cha akiba na mikopo (SACCOS) ili kuweza kujikopesha mikopo yenye riba nafuu na yenye manufaa zaidi, badala ya kukopa mikopo mitaani hali ambayo imekuwa ikiwaumiza na kuwapa hasara.

Mkurugenzi huyo ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa vitabu vya uteuzi wa viongozi, changamoto za uboreshaji elimu pamoja na mikakati ya uboreshaji elimu uliofanyika kwa ngazi ya wilaya katika ukumbi wa halmashauri hiyo.

” Walimu mmekuwa mkikumbwa na mikopo yenye riba kubwa, mikopo ya mtaani unakuta unapewa ml. 1 lakini matejesho yake pamoja na riba unakuta inaweza fika ml. 1.5 huku wengine wakikabidhi kadi zao za benki kama dhamana kitu ambacho ni kujitia umasikini”.

Amesema alipofika katika halmashauri hiyo ya Ludewa aliona kuna haja ya kuanzisha mfuko wa akiba na mikopo kwa watumishi wa idara mbalimbali ambapo kwa sasa mfuko huo umefikia katika hatua nzuri huku watumishi hao wakiendelea kunufaika.

Ameongeza kuwa kilichofanyika kwa watumishi wa idara hizo angependa kuona kinafanyika pia kwa walimu kwani wanapoenda kukopa mitaani huwa wanakuwa wenyewe lakini linapotokea tatizo naye amekuwa akihusika hivyo ni vyema kuanzisha mfuko huo utakaoweza kuwainua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *