
Timu ya ukaguzi kutoka Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu ikiwa katika ukaguzi vyanzo vya maji ilishiriki pia katika kikao baina ya wananchi na Madiwani wa Kata za Tonga na Mzumbe ambapo mbali na kutoa elimu ya utunzaji maji pia walipokea malalamiko ambayo waliahidi kuyatafutia ufumbuzi.
Katika ukaguzi wa siku mbili kuanzia leo Ijumaa Septemba 23, 2022 uliofanyika katika maeneo yanayozunguka Mto Ngerengere ambapo pia humwaga maji Mto Ruvu ambao ndiyo tegemeo la chanzo cha maji kwa wakazi wa miko ya Dar es Salaam na Pwani.

Bodi ya Wami Ruvu kupitia wataalamu wake mbalimbali imeahidi lkufanyia kazi malalamiko ambayo yametolewa na wananchi ambao wameomba zoezi la usimamishaji matumizi mengine ya maji katika vyanzo lilihitaji kushirikisha ngazi za chini ili wataalamu wapewe ushirikiano wa kutosha kutekeleza majukumu yao.
Akizungumza katika kikao hicho mmoja wa wananchi ambaye hakutaka jina lake kuandikwa ameomba makatazo yote au maelekezo yote juu ya matumizi ya maji yatolewe kwa maandishi na yapelekwe katika serikali za mitaa ili viongozi watambue na watoe elimu kwa wananchi juu ya utunzaji vyanzo vya maji.
Aidha wananchi hao waliomba wakulima na wafugaji wote kutambuliwa na kutathimini mazao yaliyo ndani ya hifadhi ya mto ili wapewe fidia na pia wapewe chanzo mbadala cha kunyweshea mifugo kwani wanachangia kupitia ufugaji huchangia miradi ya maendeleo.
