Naibu Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe amefanya kikao na Balozi wa Comoro nchini Tanzania Dr. Ahamada El Badaoui Mohamed
Mazungumzo hayo yamefanyikia Jijini Dodoma Pamoja na Wafanyabiashara kutoka Comoro kwa ajili ya kuona namna ya kupata Bidhaa mbalimbali ambazo wanazihitaji katika nchi yao na hasa kwenye upande wa chakula

Amesema wameongea na Balozi huyo na wanauhitaji wa nafaka mbalimbali pamoja na Vifaa vya ujenzi kwa uwezo wa Uzalishaji hasa Katika Mazao mbalimbali ambapo wanataka kutatua changamoto ya kukosa Masoko kwa Wakulima na hasa Kwenye Mazao ambayo yanahitajika katika nchi ya Comoro
” Mheshimiwa Balozi tulikuwa tumeongea naye na wanajitaji sana chakula mchele, nyama ya ng’ombe na kuku. pia wanahitaji maziwa pamoja na simenti kwa maana ya vifaa vya Ujenzi, sasa Tanzania sisi kwa uwezo wetu wa Uzalishaji katika Mazao mbalimbali.nadhani ni muda mwafaka sasa kutatua changamoto ya kukosa masoko kwa Wakulima wetu na hasa kwa mazao haya ambayo yanahitajika katika nchi ya Comoro hasa mchele “

Pia amesema Asilimia kubwa ya Wafanyabiashara Tanzania hususani Wakulima wanalalamika kwa Ukosefu wa soko la Bidhaa kama nafaka lakini kwa sasa watu wa Comoro wanahitaji Tani nyingi za mchele kwa kila mwezi na mpaka sasa Soko lipo wazi
“Wafanyabiashara wetu hasa wakulima mara nyingi wanalia na Soko la Bidhaa zao hasa mazao ya chakula na ya Biashara, Pia tunakosa Soko na nimefurahi wenzetu kutoka Bodi ya nafaka mchanganyiko tunahangaika sana kuhusu soko la mazao mbalimbali ikiwemo mahindi, maharage, mchele nakadhalika,
“Sasa wenzetu wa Comoro wanahitaji takribani Tani Milioni 1 hadi 2 za mchele kila mwezi na soko lipo wazi ni mwezi sasa tangu tulipowasiliana lakini bado hatukupata mwafaka na ndo maana tumekutana leo ili tujadiliane , kwanza kupata soko hili la wenzetu kutoka Comoro”

Kwa Upande wake Balozi wa ComoroDr. Ahamada El Badaoui Mohamed amesema mpaka sasa soko lipo na amewakaribisha Wafanya iashara na wakulima kupeleka Bidhaa mbalimbali Comoro kwani bidhaa hizo zinahitajika sana kwenye nchi yao na anampongeza Rais Samia kwa kufanya ukombozi hasa kwenye Sekta ya uchumi kwani Tanzania pamoja na comoro ni kama ndugu
“Soko lipo na watanzania wote karibuni Comoro mchele, ndizi, cassava, nyama na maziwa ni vitu ambavyo vinahitajika sana sasa Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan anapenda kufanya ukombozi kwenye uchumi kwani Comoro na Tanzania ni Ndugu. Waziri wa Tanzania karibu sana Comoro kwa ajili ya Biashara”.amesema Balozi Ahamada