MAKAMU WA RAIS AFANYA MAZUNGUMZO NA USAID NEW YORK.

NEW YORK.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
Philip Mpango akifanya Mazungumzo na Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya
Kimataifa la Marekani (USAID) Bi. Samantha Power, Mazungumzo yaliofanyika
Jijiji New York Nchini Marekani
.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Shirika la
Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) Bi. Samantha Power,
Mazungumzo yaliofanyika Jijiji New York Nchini Marekani .
Katika Mazungumzo hayo Makamu wa Rais ametaja juhudi mbalimbali
zinazofanywa zinazofanywa na serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha
sekta ya afya hususani Afya ya mama na mtoto kwa kuanzisha programu
mbalimbali za kuokoa Maisha ya Mama na mtoto kwa kushirikiana na wadau
ikiwemo programu ya M- Mama.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
Philip Mpango akimkabidhi zawadi ya picha ya Wanyama wakubwa watano
ulimwenguni wanaopatikana Tanzania Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya
Kimataifa la Marekani (USAID) Bi. Samantha Power mara baada ya
Mazungumzo yao yaliofanyika Jijiji New York Nchini Marekani.

Amesema serikali imeendelea kushirikiana na wadau wa afya katika kuboresha huduma za afya na kuongeza juhudi katika
ujenzi wa miundombinu ya afya ikiwemo vituo vya afya pamoja na hospitali.
Makamu wa Rais ameishukuru serikali ya Marekani kwa kushirikiana na
Tanzania katika kupambana na Uviko 19 kwa kutoa msaada wa dozi milioni 5
za chanjo ya ugonjwa huo.
Amesema serikali imeweka mkazo katika kuboresha mazingira ya uwekezaji
kwa kuweka sera rafiki na kuunganisha taasisi zinazohusika na uwekezaji ili
kuondoa urasimu kwa wenye nia ya kuwekeza Tanzania. Pia Makamu wa Rais
ametaja juhudi zinazofanywa katika kuboresha miundombinu ya usafirishaji
pamoja na nishati ili kuwa na mazingira rafiki kwa wawekezaji.
Katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, Makamu wa Rais amekaribisha
USAID kushirikiana na Tanzania katika kupata teknolojia rafiki ya mazingira
itakayowezesha wananchi kuendelea na shughuli za kiuchumi na kijamii bila
kuathiri mazingira.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Shirika la
Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) Bi. Samantha Power mara
baada ya Mazungumzo yao yaliofanyika Jijiji New York Nchini Marekani.

Kwa upande wake Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani
(USAID) Bi. Samantha Power amesema Shirika hilo litaendelea kushirikiana na
Tanzania katika kuunga mkono juhudi mbalimbali za mageuzi hususani katika
sekta ya afya na kilimo.
Bi Samantha ameongeza kwamba shirika hilo linaiunga mkono Tanzania
katika kuifanya kuwa tegemeo la upatikanaji wa chakula kwa kuwezesha
kupatikana kwa mbolea ya gharama nafuu itakayosaidia kuinua sekta ya
kilimo.
Katika hatua nyingine Makamu wa Rais ameshiriki Mjadala uliobeba ajenda ya
Demokrasia ulioandaliwa na Shirika la la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani
(USAID) na kushirikisha wakuu wa nchi na serikali pamoja na wakuu wa
mashirika ya kimataifa , mjadala uliofanyika kando ya Mkutano wa Baraza Kuu
la 77 la Umoja wa Mataifa (UNGA) Jijini New York nchini Marekani.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
Philip Mpango akichangia mjadala wa Ajenda ya Demokrasia uliowakutanisha
Wakuu wa nchi na serikali pamoja na wakuu wa mashirika ya kimataifa
uliofanyika kando ya Mkutano wa Baraza Kuu la 77 la Umoja wa Mataifa
(UNGA) Jijini New York nchini Marekani.

Katika majadiliano hayo , Makamu wa Rais amesema serikali ya Tanzania
imeweka mkazo katika mageuzi ya kuimarisha uchumi na utawala wa
kidemokrasia kwa kuhakikisha sekta binafsi inashiriki vema katika ujenzi wa
taifa pamoja na kushirikiana na wadau wa kimataifa katika kufikia maendeleo.
Makamu wa Rais yupo nchini Marekani kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa
Baraza Kuu la 77 la Umoja wa Mataifa (UNGA).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *