SPIKA DKT. TULIA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA JAPAN NCHINI.

Dodoma.

Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi Mpya wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yasushi Misawa leo tarehe 21 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.

Mhe. Spika alimpongeza Balozi huyo kwa kutenga muda wa kwenda kujitambulisha na kueleza mafanikio makubwa yaliyopatikana kupitia uhusiano wa muda mrefu baina ya Tanzania na Japan hususan miundombinu ya barabara, umeme na miradi ya kijamii.

Kwa upande wake Mhe. Balozi Misawa alimshukuru Mhe. Spika kwa kukubali kukutana nae na ameahidi kuendeleza uhusiano mwema baina ya nchi zote mbili.

Aidha, amemhakikishia Mhe. Spika kuwa Ubalozi wake pamoja na Shirika la Japan Agency for International Cooperation (JAICA) utaendelea kusaidia kuchochea maendeleo ya Tanzania kwa ujenzi wa zahanati, mabweni na uchimbaji wa visima vya maji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *