HALMASHAURI ZINAZOKUSANYA KUANZIA BILIONI 5 ZIELEKEZE 10% KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA.

OR -TAMISEMI.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa amewaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri zinazokusanya mapato ya ndani ya zaidi ya Sh bilioni 5 kwa mwaka kutenga asilimia 10 ya fedha za maendeleo kuboresha miundombinu ya barabara za lami za mitaa.

Bashungwa ametoa maelekezo hayo leo Septemba 21, 2022 bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali msingi la Mbunge wa Ukonga, Jerry Slaa(CCM).

Slaa alitaka kupata kauli ya Serikali juu ya kutenga fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya kujenga barabara za lami katika mitaa ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Akijibu swali hilo, Bashungwa amesema halmashauri zote ambazo zinakusanya kuanzia Sh bilioni 5 ya mapato ya ndani kutenga asilimia 10 kati ya asilimia 60 zinaoelekezwa kwenye miradi ya maendeleo kuelekezwa kuboresha miundombinu ya barabara za mitaa.

“ Nimeshatoa maelekezo kwa halmashauri ambazo zinapaswa kutenga asilimia 60 ya mapato ya ndani kwa ajili ya Miradi ya maendeleo kuhakikisha wanatoa asilimia 10 kwa ajili ya kutengeneza barabara za mitaa ikiwemo Mkoa wa Dar es Salaam.”

Pia amezitaka halmashauri hizo kushirikiana na Wakala wa Barabara za Mijini naVijijini (TARURA) kuweka mpango mkakati wa pamoja wa kuhakikisha asilimia 10 inayotengwa, inatengeneza barabara ambazo zitaendana na uhalisia wa matumizi ya fedha.

Aidha, Bashungwa amesema halmashauri zote za Mkao wa Dar es Salaam zitanufaka na utekelezaji wa Mradi Uboredhaji wa Miundombinu katika Jiji la Dar es Salaam awamu ya pili (DMDP).

Bashungwa alikuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Kigamboni, Dk Faustine Ndugulile (CCM) aliyetaka kujua ni lini Mradi wa Dar es Salaam Metrpolitan Development Project (DMDP) awamu ya pili utaanza katika Jimbo kla Kigamboni.

Akijibu swali hilo, Bashungwa amesema Serikali inaendelea kufanya mazungumzo na benki ya Dunia juu ya mkopo wa fedha kwa ajili ya mradi wa uboreshaji wa miundombinu katika jiji la Dar es Salaam awamu ya pili ambapo halmashauri zote za Mkoa wa Dar es Salaam zitanufaika pamoja na Jimbo la Kigamboni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *