
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Mhandisi Hamad Masauni (Mb), kwa
Mamlaka aliyonayo chini ya Kifungu cha 2 cha Amri ya Uanzishwaji wa Bodi ya Shirika la
Uzalishaji Mali ya Magereza, iliyofanyiwa Marekebisho Mwaka 2022 (The Prisons Corporation
Sole Board (Establishment)(Ammendment) Order, 2022), amewateua Mwenyekiti, Katibu na
Wajumbe 10 wa Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza (SHIMA).
Waziri Masauni amemteua Inspekta Jenerali wa Polisi (Mst), Said Ally Mwema kuwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza. Pia, amemteua Bw. Moremi
Marwa, kuwa Katibu wa Bodi hiyo.
Aidha, Waziri Masauni amewateua Wajumbe wa Bodi hiyo kama ifuatavyo:-
- Bw. Emmanuel Akunay – Mjumbe
- Bw. Fuad Jaffer – Mjumbe
- Bw. Isaack Mazwile – Mjumbe
- Bw. Salim Aziz Salim – Mjumbe
- Mhandisi Theofilo Bwakea – Mjumbe
- Bi. Wanja Mtawazo – Mjumbe
- ACP John Itambu – Mjumbe
- Bw. Raymond William Mndolwa – Mjumbe
- Bw. Revocatus Rachel – Mjumbe
- Bi. Fatma Mangunda – Mjumbe
Uteuzi huo umeanza tarehe 20 Septemba, 2022.
Imetolewa na:-
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi