20 WAPITISHWA KINYANG’ANYIRO UBUNGE WA AFRIKA MASHARIKI

Wagombea 20 wamepitishwa Kugombea katika Uchaguzi wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka katika Vyama vya Siasa nchini vilivyokidhi Vigezo ambavyo ni CCM, Chadema, Cuf na Act Wazalendo.ikiwa ni Baada ya kukamilika kwa Zoezi la Uteuzi na Uratibu wa Wagombea Wa Bunge la Afrika Mashariki

Idadi hiyo imetangazwa na Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Nenelwa Mwihambi Usiku wa Leo Septemba 20, 2022 Kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika Katika Ukumbi wa Spika Bungeni Dodoma.ambapo ameeleza kuwa katika Vyama ambavyo vimekidhi Vigezo ni Chadema Pekee ambao hawajawasilisha Jina hata moja la Mgombea.

Katibu Mwihambi ametaja majina ya Wagombea ambao wamepitishwa na kukidhi Vigezo vya Kugombea.

Amesema Viti hivyo vinagawiwa kwa uwiano kutoka katika kila Chama kutokana na Idadi ya Wabunge waliopo Bungeni wa CHAMA husika.CCM inapata Viti kwa zaidi ya Asilimia 8 huku vingine vikipata Asilimia 0.05 ambao ni sawa na Kiti Kimoja.

Hata hivyo, ameeleza kupokea malalamiko kutoka kwa Baadhi ya Wagombea, huku Mgombea mmoja kutoka katika Chama Cha CUF akiwasilisha Barua ya kujiondoa na Idadi ya Wagombea kutoka katika Chama hicho ikisalia kuwa ni 11

Chama Cha Act Wazalendo wametoa Mgombea mmoja na CCM wametoa Wagombea Wanane katika Mchakato huo.

Majina ya Wagombea hao yatawasilishwa Bungeni Septemba 22, 2022 kwaajili ya kupigiwa Kura na Wabunge.

KWA UNDANI ZAIDI FUNGUA LINK HAPA CHINI KUTAZAMA VIDEOπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *