PROF.SHEMDOE AIPONGEZA KOROGWE MJI USIMAMIZI WA UJENZI, MIRADI YA AFYA

OR-TAMISEMI

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Prof. Riziki Shemdoe ameipongeza Timu ya Uendeshaji Huduma za Afya (CHMT) Halmashauri ya Mji wa Korogwe kwa usimamizi mzuri wa miradi ya afya katika halmashauri hiyo.

Ameyasema hayo leo tarehe 17 Septemba, 2022 wakati akikagua miradi ya Afya na kufuatilia zoezi la utelekezaji wa chanjo ya polio Mkoani, Tanga.

Prof. Shemdoe amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameridhia fedha zitumike kwa ajili ya ujenzi wa jengo la dharura (EMD) katika Hospitali ya Magunga Korogwe ambayo imejengwa kwa kutumia Force Account hivyo hakikisheni maeneo machache yaliyobaki yanakamilika kwa wakati.

Prof.Shemdoe amempongeza Mkurugenzi wa Mji Korogwe pamoja na Mganga Mkuu kwa kuweza kusimamia kazi ujenzi kwa wekeledi.

Prof Shemdoe amemuelekeza
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia afya na Mkurugenzi Idara ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii Dkt.Ntuli Kapologwe Ofisi ya Rais -TAMISEMI, kuhakikisha wanapeleka vifaa na vifaa Tiba vya EMD ndani ya mwezi wa kumi ili majengo hayo yaanze kutoa huduma kwa wananchi

Prof. Shemdoe amewapongeza watumishi wa Afya wa Mkoa wa Tanga hasa Halmashauri ya Korogwe Mji kwa kuvuka malengo ya uchanjaji wa Chanjo ya Polio kwa watoto.

Aidha, Halmashauri ya Mji Korogwe kwa Awamu ya Tatu sasa imeweza kufikia asilimia 119.38 ya lengo la kuchanja watoto 15,591 huku ikishika nafasi ya kwanza Kimkoa.

Prof.Shemdoe amewaagiza watumishi wa Afya katikal Mamlaka za Serikali za Mitaa kuwahudumia wananchi kwa Upendo kwa kuwa ndio waajiri wa watumishi wote nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *