
Kamisaa wa sensa ya watu na makazi nchini kwa mwaka 2022 ANNE MAKINDA amesema katika zoezi la Sensa mwaka huu jumla ya Makarani kumi walipoteza maisha kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kujiua na kuuwawa
Makinda ametoa kauli hiyo akiwa mkoani Manyara alipokutana na kamati ya sensa mkoa wa Manyara kwa lengo kupokea taarifa ya zoezi la sensa ambapo amesema.
“Mmoja wa Tabora alijinyonga mwenyewe na kuacha ujumbe,wengine walikufa kwa maradhi na mwingine aliuwawa baada ya kupata vijisenti kidogo wenzie wakadhani anae mamilioni” Amesema Makinda.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere amesema mkoa huo umefanikisha kukamilisha zoezi la sensa ya watu na makazi ambapo mkoa umeweza kizifikia zaidi ya kaya 300,000 ikiwa ni sawa na asilimia 126 ya lengo.