IGP WAMBURA ATANGAZA VITA NA PANYA ROAD” WAKAE CHONJO,NI HATARI KWAO”

Na: Debora Munisi, Dodoma

Wahalifu na wanaoshirikiana na wahalifu wametakiwa kukaa chonjo kwani serikali imeunda operesheni kabambe ya msako itakayo chunguza na kuhakikisha nchi inazidi kuwa katika hali ya utulivu na amani.


Hayo yamesemwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillius Wambura wakati akizungumza Wanahabari jijini Dodoma uliokuwa na lengo la kuelezea hatua za serikali katika hali ya ulinzi na usalama kufuatia matukio ya kihalifu hapa nchini.


” mambo waliyokwisha kuyafanya hayakubaliki na hatutakaa tukubali jambo hili lijirudie, Wakae Chonjo huu ni wakati mbaya na mgumu kwao, ninachikifikiria sijui kama hawa wahalifu wanajua kupambana na nani, mimi ninachokijua kwa uhalifu huu uliopelekea madhara kwa wananchi wa Tanzania sasa serikali kupitia Jeshi la polisi haijawahi kushindwa na mhalifu yeyote, hakuna mhalifu yeyote aliyewahi kushindana na serikali akashinda”


“tunazuia kwa operesheni ya misako ambayo inatanguliwa na Inteligense maalumu ili kuhakikisha wananchi wote wanakuwa kwenye usalama wakati tunaendelea na operesheni zingine za ukamataji wa wahalifu hao, mpaka sasa tumeweza kukamata idadi kubwa ya
“kutokana na taharuki kubwa iliyotokea ya kiuhalifu ya kihalifu iliyofanywa na wahalifu wanamekwenda kwa majina ya Panya Road nichukue nafasi hii kuwapa pole wananchi wote waliopata majeraha na kuibiwa mali zao lakini kwa wale wote ambao wameteseka kwa hofu na wale wote wanaoendelea kuteseka na hofu hadi leo”
Ameonya watu wote wenye dhamira ya kujihusisha na matukio yoyote ya uhalifu yanayoweza kuvuruga amani ya nchi kuacha haraka iwezekanavyo
“wahalifu waliohusika kwenye uhalifu uliopita, na wale waliopanga mbinu mbalimbali za uhalifu au wengine wanaojipanga kwenda kufanya uhalifu ama kwa kukaidi maelekezo yanayotolewa na Jeshi la Polisi pamoja na Serikali, nachukua nafasi hii kuwaonya, ninawaonya sana,”
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Masauni amesema tayari wamekwisha weka mpango wa kupambana na wanaovuruga amani ya nchi(Panya Road) kwani uchunguzi umebaini wahusika wakuu ni wafungwa waliomaliza muda wao gerezani.

“Serikali haichukulii uhalifu uliotokea kwa wepesi bali tumeshaanza kufanya mpango wa kupambana na wahalifu wote waliohusika(Panya Road) na kushiriki katika uhalifu huu kwa kukamatwa haraka iwezekanavyo”


Hata hivyo, amesema Suala la Ulinzi limeboreshwa kuanzia ngazi ya kata na jukumu la kulinda amani ya nchi ni kwa raia wote hivyo jamii inapaswa kuripoti vitendo hivyo vya kiuhalifu sehemu sahihi ambayo ni Jeshi la Polisi.
“Na pia uchunguzi umebaini baadhi ya wafungwa waliomaliza muda wa kifungo chao ndio wanaoenda kuwashawishi vijana wengine mtaani hivyo niwaombe wananchi mtoe ushirikiano na kwa ngazi zote hapa nchini kuanzia ngazi ya kata ili nchi yetu ibaki salama”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *