BALOZI WA UHOLANZI NCHINI AKUTANA NA WAZIRI AWESO

Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania (Ambassador for the Embassy of the Kingdom of Netherlands) Mhe. Wiebe de Boer amefika ofisi ndogo Wizara ya Maji Dodoma kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akiwa pamoja na Katibu Mkuu Eng.Anthony Sanga ambapo kwa pamoja wamejadili maswala mbalimbali yanayohusiana na Sekta ya Maji kati ya Nchi ya Tanzania na Uholanzi.

Nchi ya Uholanzi kwa muda mrefu imeendelea kuwa na mdau mkubwa kwa sekta ya Maji kwa nchi ya Tanzania na kwa pamoja Balozi na Waziri wa Maji wamekubaliana kudumisha ushirikiano huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *