DKT. ABBAS ATOA SIKU SABA KWA WATENDAJI BMT

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, ametoa siku 7 kwa watendaji wa Idara ya Michezo kukamilisha nyaraka za miradi yote iliyoko chini ya Idara hiyo la sivyo kila mhusika atabeba mzigo wake.

Dkt. Abbasi ametoa agizo hilo leo hii alipokutana na watendaji wote wanaosimamia sekta ya michezo nchini kuanzia Idara ya Maendeleo ya Michezo iliyoko Wizarani, Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya na Baraza la Michezo (BMT).

“Kuna changamoto kubwa sana za kiutendaji zilizobainika katika Idara ya Maendeleo ya Michezo kiasi cha kukwamisha miradi mingi nimekuja kuwaambia hapa nyie ndio wataalamu sisi tunatafuta hela kuna mabilioni ya fedha Serikali imetenga kila nyaraka unayouliza kazi zianze unaambiwa bado, kila kitu unachohitaji ukapewe hela Hazina hakijaandaliwa, sasa tumefanya mabadikiko ya uongozi wa juu wa Idara hii tunataka sasa kazi na matokeo na sio blah blah nyingi,” alisema Dkt. Abbasi.

Mtendaji Mkuu huyo wa Wizara ametoa siku saba kwa watendaji wanaokaimu katika Idara hiyo kukamilisha nyaraka hizo ikiwemo miradi ya ujenzi wa viwanja vya kupumzika wananchi, shule 56 za michezo na ukarabati wa viwanja mbalimbali vya michezo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *