BUNGE LAPITISHA MUSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO YA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA MAJI

Leo tarehe 15 Agosti, 2022 Bunge limepitisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji ya mwaka 2022 (The Water Resources Management Act, 2022).
Kupitishwa kwa sheria hii kutaimarisha Bodi za mabonde ya Maji katika kusimamia Rasilimali za Maji nchini vilevile kuimarisha uhifadhi wa Vyanzo vya Maji nchini ili kuhakikisha upatikanaji endelevu wa Maji majumbani na shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

Wabunge mbalimbali wakichangia Muswada huu wamempongeza Mheshimiwa Waziri wa Maji Jumaa Aweso kwa kutambua umuhimu wa utunzaji, uhifadhi na uendelezaji wa Rasilimali za Maji wakieleza kwamba Muswada huu umekuja wakati sahihi ambapo kuna ongezeko kubwa la mahitaji ya Maji ikiwa kiwango cha Rasilimali za Maji kiko palepale.

Waziri Aweso ameahidi mbele ya Bunge kuendelea kutoa elimu na ushirikwaji kwa wananchi kuhusu utunzaji na uhifadhi wa Rasilimali wakati akijibu hoja mbalimbali.
Mwisho amewashukuru waheshimiwa wabunge kwa kuunga mkono muswada huu kwa asilimia mia na kuahidi kuzingatia maoni, mapendekezo na ushauri wao katika Utekelezaji wa Sheria mbalimbali zinazohusiana na uhifadhi na utunzaji wa vyanzo vya Maji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *