KATIBU TAWALA DODOMA AKABIDHI GARI LA KUSAIDIA WAGONJWA HALMASHAURI YA KONGWA KWA MSAADA WA USAID

Na: Deborah Munisi

.
Katibu tawala Mkoa wa Dodoma Bi. Fatuma Mganga amemtaka mganga mkuu kutathmini mwenendo wa utendaji kazi na kupanga mipango mikakati itakayosaidia kufikia asilimia 95 iliyowekwa na wizara ya afya.
Wito huo umetolewa katika hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa vya afya pamoja na gari aina ya Land Cruiser lililotolewa na mradi wa USAID Afya Yangu unaohusika kutoa huduma ya Hafua za VVU, Afya ya uzazi na hafua za Uviko 19 katika halmashauri na mikoa ambapo ametanguliza shukrani kwa shirika hilo kwa kutoa fari hilo litakaloenda katika halmashauri ya Kongwa sambamba na majokofu yatakayoenda wilaya ya Chamwino.
“Kwahiyo halmashauri ya Bahi,Kondoa Dc na Kondoa Tcninyi ndo ambao mnaturudisha nyuma sasa mganga mkuu kwa wakati wako ukakae na CHMTs mpange mikakatiili tuweze kufikia asilimia 95 tuliyoelekezwa na wizara”
“Kiongozi ukipewa kipande chako halafu hufikii malengo kiongozi maana yake ni kutosha katika nafasi na kutosha katika nafasi ni kufikia malengo uliyopewa kama hufikii malengo ina maana hutoshi katika hiyo nafasi, uongozi ni neema tumepewa kutoka kwa mungu tunapaswa kuitumikia ili iweze kutosha.

Aidha amewataka watakao tumia gari hilo kutumia kwa kazi husika ili kuweza kufikia malengo na amepongeza mradi huo kwa kuwa mstari wa mbele katika kipindi cha mambambano ya UVIKO 19 kwa kutoa Oksijeni na kwa kuongoza kufikia asilimia 100 katika kuchanja chanjo hiyo .
“Sisi tunaokwenda kupewa gari likafanye kazi kusudiwa, tukatunze gari letu ili na gari hili likazae matunda tunategemea kongwa kwasababu mmepewa hili gari mkawe vinara iwe ni kwenye upimaji, self test na kufikia wananchi kweye mikutano inayofanyika huko kijijini hivyo muwe vinara”.


“Wakati ule wa uviko 19 ikiwa imepambamoto ilikuwa shida kubwa ni Oksijeni kwa ajili ya wagonjwa na walipokuja tuliwashirikisha na tukashirikiana nao kwenye hospitali yetu ya mkoa,na wadau hawa ni wadau wanaoshughulika na maisha yetu, wadau hawa ni wakubwa Kwahiyo mimi niseme kwa niaba ya serikali ya mkoa ninawashukuru sana na kama inavyofahamika oksijen siyo tu kwaajili ya Uviko 19 bali inatumika pia kwa mambo mengi kwahiyo wameshatusaidia pakubwa.”

Kwa upande wake Dkt. Sajida Kimambo ambaye ni mkurugenzi mkazi wa shirika la EGPAF Tanzania hilo Dkt. Sajida Kimambo amesema lengo la kutolewa gari hilo ni ili kurahisisha na kusaidia wasimamizi wa afya katika ngazi ya wilaya ili waweze kufikia maeneo ambayo ni changamoto kufikika kwa urahisi na kuongeza ufanisi wa kazi.


“tukikutana na wadau tunajadili ili kujua changamoto na maendeleo ya mradi hivyo vifaa hivi tulivyovitooa katika halmashauri hizi ni ili kuweza kusaidia wasimamizi wa huduma hizi za afya tunafahamu kuna maeneo ambayo yako pembezoni ambayo ciyo rahisi kufikika hivyo kwa gari hili litahakikisha wanafikia wananchi kutoa huduma ili kuweza kutoa tathmini ya mradi”

Naye kaimu mganga mkuu mkoa France Guligo amelishukuru shirika hilo kwa katika kuboresha huduma ufuatiliaji na usimamizi katika ngazi ya halmashauri.
“kwanza nishukuru huu mradi wa USAID Afya Yangu katika kuboreshahuduma na usimamizi katika mkoa huu hususani katika halmashauri ya Kongwa piah kuna friji tumepokea ambazo zitakuwa hususani kwa ajili ya kutunza sampuli na tunashukuru piah kuwa zitaendelea kuboresha hilo eneo katika mkoa wetu”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *