RAIS SAMIA AANDIKA HISTORIA MRADI WA MAJI MKINGA-HOROHORO

Wizara ya Maji imesaini mkataba na Mkandarasi STC wa kuanza rasmi utekelezaji wa Mradi Mkubwa wa maji MKINGA – HOROHORO wenye thamani ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 34 .
Mradi huu unatarajiwa kutekelezwa ndani ya miezi 12 kuanzia mwezi Septemba,2022 na utahusisha ulazaji wa bomba kubwa la kutoa maji mto zigi uliopo wilaya ya Tanga mjini hadi wilayani Mkinga na na kazi nyingine ya ulazaji wa mabomba ya kusambaza huduma ya majisafi kwa wakazi wa wilayani humo, ambapo zaidi ya wananchi 68,000 watanufaika na mradi huo.

Aidha, Waziri Aweso amewasisitiza wakandarasi waliosaini mkataba huu kufanya kazi kwa weledi mkubwa kwani wana Mkinga wameteseka na changamoto ya Maji kwa muda mrefu sana na Mradi huu ni tumaini na faraja yao.

Katika hatua nyingine,Wananchi wa Wilaya ya Mkinga wakiongozwa na Mbunge wao Mhe.Dastan Kitandula wametoa shukrani zao za dhati kwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha ujio wa Mradi huu unaokwenda kumaliza kabisa changamoto ya Maji Mkinga.

Hafla hiyo ya utiaji saini Mkataba wa utekelezaji mradi wa maji Mkinga – Horohoro imefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga na kushuhudiwa na Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Omary Mgumba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *