NHC YADHAMIRIA KUBADILISHA MAISHA YA WATANZANIA

Meneja wa Habari na Uhusiano wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Ndg: Muungano Saguya ameishukuru Vodacom Tanzania kwa kuunga mkono Shirika hilo kwa kununua nyumba kwaajili ya matumizi yao binafsi.

Ametoa Shukrani hizo wakati wa hafla ya kukabidhi Nyumba kwa mshindi wa Nyumba kutoka kwenye Kampeni ya Mpesa imeitika, leo September 09, 2022

Pia ametoa wito kwa watanzania kuendelea kujitokeza kuhakikisha NHC inafika mbali

Amesema NHC wana lengo la kubadilisha maisha ya watanzania kushirikia na Vodacom ili kuhakikisha watanzania wanapata nyumba nzuri na bora,


” kipekee nichukue nafasi hii kishukuru vodacom Tanzania LTD kwa kuweza kujua hilo kwamba sisi ni brand kubwa katika suala zima la makazi na ndio maana waliweza kutuunga mkono kwa kuwa wanunuzi wa nyumba hii ambayo wanaenda kuitumia kadri mlivyo sikia , kwaiyo tunaimani kwamba Vodacom Tanzania kwenye program zenu mnazo fanya mzuri kabisa za kubadilisha maisha ya watanzania mtaendelea kutushika mkono shirika la nyumba la taifa ili tuweze kuwa pamoja na kufanya watanzania waweze kumiliki nyumba “


Aidha amesema katika mradi wa iyumbu wameweza kujenga nyumba nyingi na nyumba hizo zipo hatua za mwisho kukamilika na pia baadhi ya wanunuzi ambao tayali wameshaweza kuweka fedha zao za awali

Ametoa wito kwa watanzania waweze kujitokeza kwa wingi na wanaahidi mradi huo unakwenda kukamilika mwezi Octoba 2022

ameeleza Nyumba hizo ni za kisasa na zina mahitaji yote ya muhimu ikiwemo maji, umeme na barabara
” katika mradi huu wa iyumbu tumejenga nyumba takribani 300 ni nyumba ambazo sasa zipo asilimia 95 kukamirika wapo wanunuzi ambao wameshaweka fedha zao za awali, tuinaishukuru Vodacom walilipa kabisa fedha zao na ndio maana tunawakabidhi asubuhi hii nyumba pamoja na hati za makabidhianao na tunatoa wito sasa kwa wateja ambao walikwisha lipia sehemu ya manunuzi ya nyumba zao hapa tunaomba wakamilishe malipo yao kwasababu mradi huu unakwenda kukamilika mwezi octoba 2022
” tayari tumesha wakabidhi wateja wetu nyumba zao ambazo zimekwisha kukamilika na wanaendelea kuishi kama ambavyo mshindi wetu wa leo atakavyo endelea kuishi katika nyumba yake mpya


Pia amesema katika mwezi huu shirika la nyumba la taifa wana mradi mkubwa wa kwenda kutekeleza na ni mradi mkubwa ambao unagharimu nyumba takribani 5000 ambao utasambaa katika mikoa mbalimbali hapa nchini lakini kwa upande wa Dar es saalam kutakuwa na asilimia 50 kwa kuanza na eneo la kawe na watanzania wote watakuwa na uwezo wa kununua na tayali hadi hivi sasa kuna baadhi ya watanzania wamesha jiandikisha kwaajilibya kununua nyumba hizo


” Shirika la nyumba la taifa linakwenda kutekeleza mradi mkubwa unaoitwa Samia Housings Skin ni mradi wa nyumba takribani 5000 utakao enezwa katika mikoa mbalimbali nchini lakini kutokana na mahitaji ya nyumba Dar es saalam utakuwa na asilimia 50 ya nyumba hizo zitaenda kujengwa mwezi huu tunaanza na nyumba 500 eneo la kawe ni nyumba ambazo watanzania wenye kipato cha chini wanaenda kuzimiliki kwa maana ya kununua nyumba za gorofa 10 na tayali hivi ninavyo zungumza watanzania mbalimbali wamesha jiandikisha kwenye ofisi za National housing kuonyesha nia ya kununua nyumba hizo “

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *