KATIBU MKUU KIJAZI AKOSHWA NA UBUNIFU WA MAKAMPUNI KWA NHC

Wizara ya Ardhi, nyumba na maendeleo ya Makazi imeyapongeza Makampuni ya Vodacom Tanzania na GSM kwa kutoa zawadi ya nyumba kutoka NHC kwa mshindi wa “MPesa imeitika”


Hayo yamesemwa na Karibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na, Maendeleo ya Makazi mapema leo 09, September 2022 wakati wa kukabidhi zawadi ya mshindi wa Mpesa imeitika ambapo Vodacom kushirikiana na GSM wameweza kumkabizi mshindi huyo nyumba kubwa yenye kila kitu ndani.


” nawapongeza Vodacom na GSM kwa kujipanga kwa pamoja kuweza kutoa nyumba ikiwa na samani zake, suala la umiliki wa nyumba hasa nyumba za makazi ni kitu muhimu sana kwa maisha ya binadamu nipende kuwashukuru Vodacom kwa ubunifu huu ambao mmeufanya mmetoa zawadi tofau titofauti nimeambiwa kulikuwa na bodaboda,
bajaji lakini mkaona haya yote hayatoshi shindano haliwezi kunoga bila kuwa na nyumba kwakweli huu ni ubunifu wa aina yake na niwapongeze sana kwa kulifikiria hilo naamini ni mara ya wanza kwa vodacom kufanya hivyo na sisi wizara tunawaunga mkono kwa ubunifu huo” amesema Dkt. Kijazi


Pia amesema wao kama wizara wamezoea kuona matukio kama haya yanayo fanywa na Vodacom pamoja na GSM wanayaonaga tu katika mataifa ya nje na ilikuwa inaeleweka kwa mashirika kama haya hayawezi kusimama na wala kuwa na ubunifu pasipo kuwa na msaada kutoka mataifa ya nje lakini kutokana na tukio ambalo wamelifanya siku ya leo unathibitisha kwamba watanzania wanaweza kuliko hata hao wa nje


” kikubwa zaidi kinacho tupa moyo sisi kama serikali na pia kama wizara ni kwamba tumezoea kuona matukio kama haya yanayofanywa na vodacom hasa viongozi kutoka mataifa ya nje na kulikuwa na dhana imejengeka kwamba mashirika kama haya hayawezi kusimama au hayawezi kuwa na ubunifu bila kuwa na wenzetu kutoka mataifa ya jirani au mataifa ya mbali lakini kwa tukio la leo litatuthibitishia kwamba watanzania tunaweza na tunao uwezo kuliko hata hao wenzetu wa nje, kwaiyo tunakupongeza sana mkurugenzi mkuu wa vodacom kwa kuwa mbunifu kwa kutudhibitishia watanzania na kimataifa kwamba tunaweza ”


Aidha amesema kuwa ubunifu huo ambao vodacom wameufanya unaendana na dira ya wizara ambayo inalenga kumfanya kila mtanzania kuwa na uhakika wa umiliki wa nyumba na sio tu nyumba bali nyumba bora na ambayo ipo kwenye makazi endelevu
” ubunifu huo ambao mmeufanya unaendana na adhma na dira ya wizara inayolenga kumfanya kila mwananchi kuwa na uhakika wa umiliki wa nyumba lakini siotu suala la nyumba lakini nyumba bora ambayo ikobkwwnye makazi endelevu na ya uhakika.


” kwahiyo ukiangalia ubora wa nyumba hii ambayo imejengwa na National Housing lakini ukiangalia makazi yanayozunguka nyumba hii nadhani yanaridhisha kwamba nyumba ni bora na makazi yaliyopo niendelevu, kwahiyo pia nichukue nafasi hii kuwashukuru sana wenzetu wa vodacom kwa kuchukua uwamuzi wa kuja kununua nyumba hapa National Housing kununua nyumba kwaajili ya mshindi wetu”

Aidha amesema wao kama serikali itaendelea kuwaunga mkono hasa katika jitihada zao kwa lolote lile ambalo serikali itaweza kushiriki na hii yote ni katika kuendeleza maisha safikwa kila mtanzania na kwa tukio hilo limesha fungua ukirasa mpya wa ushirikiano


“sisi wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi tunawaunga mkono na tutaendelea kuwaunga mkono katika jitihada zenu kwa lolote lile ambalo mnafikiri tunaweza tukashirikiana na vodacom katika kuendeleza maisha ya mtanzania tuko tayari kufanya hivyo na nina imani kwamba tukio la leo limefungua ukurasa wa ushirikiano”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *