WATANZANIA WATAKIWA KUSALIMISHA SILAHA HARAMU KWA HIYARI


Serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani ya nchi imetoa wito kwa wananchi kusalimisha silaha haramu kwa hiyari yao ili kudumisha, na kulinda amani na utulivu wa nchi.
Wito huo umetolewa na naibu waziri wa mambo ya ndani Jumanne Sagini Ambaye ni mwakilishi wa mgeni rasmi Waziri wa wizara ya mambo ya ndani Mhandisi Hamad Masauni katika uzinduzi wa kampeni ya uzinduzi maalumu ya kusalimisha silkaha haramu kwa hiyari iliyofanyika katika uwanja wa mashujaa jijini dodoma mapema leo yenye lengo la kurasimisha silaha haramu kwa hiyari ili kuendelea kuimarisha ulinzi, amani na usalama hapa nchini.
“Tukio hili ni kielelezo cha jitihada zinazofanywa na Serikali yetu katika kuunga mkono mikakati ya Jumuiya ya Kikanda na Kimataifa katika kupambana na tatizo la uzagaaji wa silaha haramu”.
Amewatoa hofu wamiliki watakao salimisha silaha hizo kwa hiyari yao kwa kuwa serikali imetangaza msamaha kwa watakao salimisha katika vituo vya polisi, ofisi za serikali za mitaa, na ofisi za watendaji wa kata.

“Kampeni hii itasaidia kuwatoa hofu wananchi kujitokeza kwa wingi kurasimisha silaha haramu wanazomiliki kwa kufuata Sheria iliyowekwa kwa kipindi hiki Cha msamaha, hatachukuliwa hatua zozote za kisheria na hatashitakiwa mtu kwa kipindi hiki Cha September na October”
“Utekelezaji wa mpango huu utasaidia Jitokezeni kwenye vituo vya polisi, ofisi za serikali za mitaa, ofisi za serikali za watendaji wa kata, hivyo niwaombe waanchi mjitokeze kwenye ngazi hizo.”
aidha ametoa wito kwa wanao miliki silaha ambazo walikuwa wakitumia ndugu zao wakafariki kuzirejesha haraka iwezekanavyo.
“Serikali inawaomba wananchi wote wanaomiliki silaha kienyeji au kinyume cha sheria, wajitokeze kwa wingi ili watumie fursa hii ya msamaha kusalimisha silaha wanazozimiliki isivyo halali na wapo baadhi ya watu wanaomiliki silaha zilizokuwa zikimilikiwa kihalali na ndugu zao waliofariki badala ya kuzisalimisha katika Vituo vya Polisi, natoa rai kwa kundi hili kusalimisha silaha hizo kwani kuendelea kubaki nazo ni makosa makubwa kwa kuwa zinaweza kuhatarisha usalama wa raia na mali zao”.
amehitimisha kwa kuwataka viongozi mbalimbali kutoa ushirikiano ili kudumisha amani na utulivu hapa nchini.
“Silaha haramu zinachangia kwa kiasi kikubwa katika kuvuruga amani ya nchi na kudhoofisha demokrasia na uhuru wa wananchi, hivyo tunavyozindua kampeni hii tunapeleka ujumbe kuwa Serikali inataka kuhakikisha kuwa wananchi wa Tanzania wanaishi na kutekeleza kazi mbalimbali kwa amani.
“Nawataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya nchini kwa kusaidiana na Makamanda wa Polisi wa Mikoa kuongoza mpango wa uhamasishaji wananchi katika kampeni hii”.
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la polisi Tanzania IGP Camillus Wambura Amesema jambo hilo ni la dunia nzima na ni kufuatia mpango wa umoja wa mataifa na ni vyema kutumia muda huu uliotolewa kwa kuzingatia Sheria iliyowekwana kuishukuru serikali ya awamu ya sita kukubali msamaha huo.
“naishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kukubali kutoa msamaha huu ili silaha haramu zisalimishwe na hivyo kuimarisha amani na utulivu wa Taifa letu na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachoshughulikia uondoshwaji wa silaha haramu, Umoja wa Afrika na Kituo cha Kikanda cha Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Ndogo na Nyepesi”.

Aidha Amesema zoezi la kukusanya silaha hizo likikamilika silaha hizo zitateketezwa kwa uwazi kwa lengo la ustawi wa maendeleo ya nchi na kubainisha kufutiwa kwa umiliki wa silaha kwa ambao walienda kinyume na Sheria.

”katika kipindi cha Januari 2019 hadi Juni 2022, jumla ya silaha 997 zilikamatwa kutokana na oparesheni mbalimbali za kuzuia na kutanzua uhalifu na wahalifu, jumla ya silaha 52 zilizokuwa zinamilikiwa kihalali ziliibiwa kutoka kwa wamiliki ikiwa inamaanisha kuwa bado zipo silaha zinazomilikiwa isivyo halali”.

Ikumbukwe kuwa Chimbuko la la mradi wa urasimishaji wa sihala haramu umoja wa nchi huru Afrika Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi wanachama mnamo mwaka 2017 Adis Ababa Ethiopia yenye adhimio la kila ifikapo mwezi September kuwa mwezi wa msamaha kwa usalimishaji wa silaha haramu Hadi mwaka Huku mkoa wa dodoma uzinduzi wa kampeni ukienda sambamba na kauli mbiu ya “Silaha Haramu Sasa Basi Salimisha Kwa Hiari”.

Na Deborah Munisi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *