MBUNGE ULANGA ATEMBELEA MRADI WA KUSAMBAZA UMEME IFAKARA

Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mheshimiwa Salim Hasham ametembelea kituo Cha kupokea na kusambaza umeme Cha Ifakara kinachogharaimu zaidi ya Bilion moja nukta tisa( bil. 1.9)

Kituo hicho kitatumika kusambaza umeme katika Jimbo la Ulanga ambapo msimamizi wa Mradi huo Mhandisi Peter John amesema unatarajia kukamilika mwezi novemba mwaka huu.

Mhandisi John anasema kwa Sasa ujenzi umefikia asilimia sitini hivyo wanatarajia ukamilike kwa wakati kwa Sasa mafundi wote wapo eneo la kazi na wanaendelea na ujenzi.

Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mheshimiwa Salim Hasham amesema lengo la kutembelea Mradi huo ni kuona hatua iliyofikia ili kuondoa changamoto ya kukatika umeme katika Jimbo lake .

Aidha Salim ameongeza kwa kusema kupatikana huduma hiyo itachochea kuongezeka kwa wawekezaji katika sekta ya madini kutokana na sekta hiyo kuwa tegemo kubwa kwa Serikali katika ukusanyaji Mapato.

Pia Mheshimiwa Salim amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kufikisha huduma ya umeme katika Jimbo lake la Ulanga

Salim amasema Jimbo la Ulanga Lina vijiji 59 ambapo Kati ya hivyo vijiji 58 tayari vimepata huduma ya umeme na kuongeza Hali ya uchumi kwa wananchi mpoango kwa Sasa ni kupeleka umeme katika Kila kitongoji.

Kwa upande wake meneja TANESCO wilaya ya Ulanga John Rugan anasema kukamilika kwa Mradi huo licha ya itasaidia Serikali kuongeza mapato ambayo yatatokana na wananchi kuanzisha viwanda .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *