“HATUNA SABABU YA KUGOMBANA, KUWENI HURU KUTOA MAONI” WAZIRI MWIGULU

Na: Debora Munisi-Dodoma

Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Mwigulu Nchemba leo akiwa Dodoma amekutana na Waandishi wa Habari kutolea ufafanuzi wa masuala ya tozo kwenye miamala ya simu na benki jambo ambalo limekua gumzo nchini kwa kujibu kitendawili ambacho wengi wanauliza, mbona zamani hakukuwa na tozo lakini Nchi ilikua inaenda?.

“Wengine wanasema mbona zamani Nchi ilikua inaenda tu ? ni kweli kabisa Ndugu zangu zamani Nchi ilikua inaenda tu wakati wa Mwalimu Nyerere wanaosoma Shuleni walikuwa wanapewa na mayai kabisa lakini sasa jiulizeni huko Chuoni walikua wangapi ? walikua 12, walikua 7, tuulizeni wengine tuliozaliwa familia ya Watoto 11 hatukujua kama kuku ana robo, hata kipapatio kinakatwa mara tatu wote lazima muenee”

Amesema amesikia maoni ya wananchi wanaohisi serikali imefumbia macho swala hilo ambapo Amesema walikuwa wanakusanya maoni kutoka kwa Wadau mbalimbali yaliyokuwa yanalenga mambo mbalimbali na kuahidi kufanyika kazi.
“Tumesikia maoni ya Wananchi wengine walisema tupo kimya, tulikuwa kimya tukisikiliza maoni ya Wananchi, tumekutana na Watalaamu wa Kodi tumepata maoni yao maoni yamelenga maeneo mbalimbali ila kubwa ni tozo za miamala ukituma na ukitumiwa na kwenye inatozwa, tumepokea na tunayafanyia kazi na tutatoa majibu ya utekelezaji wake siku sio nyingi”

“Kuweni watulivu wakati tunashughulikia hoja hiyo, tumeona wengine wakizungusha risiti zenye viwango vya tozo wakionesha pesa iliyokusanywa kwenye Benki, tutakutana na Taasisi za Fedha tuone kuhusu hilo, Nchi hii ni yetu wala Mtu usihofie kutoa maoni, hatuna sababu ya kugombana kwenye hoja zenye mantiki”
Waziri mchemba amegusia juu ya malalamiko ya Kodi ya upangishaji wa majengo ambapo Amesema.
“Nimesikia malalamiko kuhusu kodi ya upangishaji wa majengo, hii sio sheria mpya ila utekelezaji wake umeanza mwaka huu, wengine wanasema kwanini Mpangaji apewe kazi ya TRA ya kukusanya apeleke fedha TRA, hii sio kodi ya Mpangaji, anayepaswa kulipa kodi ya kupangisha ni Mwenye nyumba na kuhusu Mpangaji anageukaje kuwa mkusanya kodi tumeipokea na tunaifanyia kazi, ni kweli inaweza kumgombanisha na Mwenye nyumba wake na kumpotezea muda”
“Sisi wote ni Watanzania hakuna aliye Mtanzania na nusu, twendeni kwenye misingi ya haki, hivi kama Mtu mwenye kima cha chini anatozwa kodi halafu kuna anayemiliki majengo anapangisha pesa karibu Tsh. Mil 60 halafu tusimtoze kodi kisa mazoea tu, wengine wanasema ‘Huyu Waziri huyu kasoma wapi huyu!?.
Amewasisitiza wananchi kuwa watulivu katika kipindi hiki nakuwahakikishia serikali imesikia kilio Chao hivyo waachekuwa na hofu ya kutoa maoni kwani wanalifanyia kazi.

Kwa upande wake waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa amesema katika bajeti ya mwaka wa fedha 2021/22 Serikali ilitoa Shilingi bilioni 117 za Tozo za Miamala ya Simu kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Afya 234 kwenye Tarafa na Kata ambazo hazikuwa na Vituo vya Afya.

Bashungwa amesema kuwa kwa upande wa elimu bila ada Serikali imehakikisha sera ya elimu bila ada katika mwaka wa fedha 2022/23 imetenga kiasi cha shilingi bilioni 346.5
“Namshukuru sana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa umahiri wake wa kuwajali wananchi wa Tanzania na kuwezesha miradi mikubwa kama hii” amesema.
Amehitimisha kwa uwaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa miradi ambayo ilipokea fedha mwishoni mwa mwaka wa fedha 2021/22 na ikamilike kwa wakati

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *