MKANDARASI AKABIDHIWA ENEO LA UJENZI WA BWAWA LENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI KUMI NA MOJA CHAMWINO

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amemtaka mkandarasi NAKUROI CONSTRACTORS, kukamilisha ujenzi wa Bwawa litakalotumika kwa kilimo cha Umwagiliaji lililopo Membe wilayani Chamwino kwa wakati uliopangwa baada ya kukabiziwa eneo la ujenzi wa mradi huo.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akizungumza na wananchi wa Membe baada ya Mkandarasi kukabidhiwa eneo la ujenzi wa Bwawa  litakalotumika katka kilimo cha Umwagiaji
Mhandisi Salehe Madebe kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji akionesha viongozi wa Wilaya ya Chamwino eneo linalokwenda kujengwa Bwawa, la Membe litakalotumika katika kilimo cha Umwagiliaji.


Mhe. Senyamule, Serikali imedhamiria kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya kilimo ili kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na uchumi wananchi kwa ujumla. “ Mkandarasi anatakiwa kujenga mradi huu kwa mwaka mmoja hivyo tunawaomba wananchi wa hapa membe kuwa wasimamizi wa huu mradi, ni wakwenu na muwe walinzi maana fedha zinazojenga mradi huu ni za kwenu.” Alisisitiza mkuu wa Mkoa.
Akiongea wakati wa kukabidhi mradi huo kwa Mkandarasi, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Gift Msuya amempongeza Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe kwa kuwa na utashi wa kuhakikisha kwamba mambo makubwa ambayo Mhe Rais anatarajia yatokee katika sekta ya kilimo yanafanikiwa kwa kiasi kikubwa na kwa viwango vya hali ya juu. “ Sisi wenyewe tumekuwa mashahidi wa mambo makubwa na mapinduzi makubwa yanayokwenda kutokea katika wizara hii ya kilimo.” Alisema

Kushoto Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Gift Msuya akimkabidhi kabrasha mwakilishi wa kampuni ya NAKUROI CONTRACTORS Mhandisi Daniel Malisa katika eneo la ujenzi wa Mradi.


Kwa upande wake Mhandisi wa Umwagiliaji wa Wilaya ya Chamwino Salehe Madebe amesema, bwawa hilo litakuwa na ujazo wa Cubic metres Milioni 5.1. Tumeweza kuweka mikakati ya kujenga bwawa hili ambalo litadumu kwa muda mrefu, bwawa ambalo litakidhi mahitaji ya kilimo cha umwagiliaji ambapo itajengwa skimu yenye ekari elfu nane, malambo ya kunyweshea mifugo na matumizi ya nyumbani.
“Naomba viongozi katika ngazi zote tushirikiane kwa pamoja kuhakikisha mradi huu unatekelezwa kwa wakati.” Alifafanua.

Mhandisi wa Umwagiliaji wa Mkoa, Raphael Laizer  akiongea na baadhi wa viongozi wa Mkoa wa Dodoma na wilaya ya Chamwino katika makabidhiano ya eneo la ujenzi wa mradi kwa Kandarasi.


Mradi wa Bwawa la Membe ni moja kati ya miradi 21 ya kilimo cha Umwagiliaji iliyosainiwa mbele ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho ya sikukuu ya wakulima nanenane yaliyofanyika kitaifa mkoani Mbeya mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *