BALOZI PROF. ADELAROUS KILANGI AWATAKA WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURSA ZA MBALIMBALI ZINAZOPATIKANA BRAZIL

Balozi wa Tanzania Nchini Brazili Mhe. Prof. Adelarous Kilangi, amewataka Watanzania kuzitumia fursa za kiuchumi zinazopatikana nchini Brazili, hasa kwenye Sekta za Kilimo, Biashara, Uwekezaji na Mifugo.

Balozi Kilangi ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Vyombo vya habari kwa njia ya Mtandao wa Zoom, kutokea nchini Brazili ambapo alitumia fursa hiyo kueleza matunda ambayo Tanzania inaweza kuyapata kupitia ushirikiano wake na Brazili.

“Miongoni mwa fursa ziliopo Brazili ni kwenye Sekta ya Kilimo hasa kilimo cha Maharage ya Soya, Mtama na Mahindi ya Njano, kuna kampuni tumewasiliana nayo kutoka China imekuja Tanzania, imeanza kulima Soya na tunatarajia itaanza kulima Maharage ya Njano na Mtama, kwa hiyo Wakulima wetu Tanzania wanaweza kuanza kulima mazao haya.” Amesema Balozi Prof. Kilangi

Kuhusiana na suala kukabiliana na Upandaji wa gharama za Mafuta na nishati Mhe. Balozi Kilangi amewashauri Wadau wa kujikita zaidi kwenye uzalishaji wa Gesi aina Ethanol ambayo imesaidia kupunguza gharama ya bei ya mafuta Brazili.

“Kwenye Mafuta na Gesi Ubalozi tulitembelea kiwanda kikubwa cha kuzalisha ETHANOL hapa Brazili, watawekeza Tanzania, tunashauri wadau waitumie fursa hii ya kuzalisha Ethanol, kwa sababu wakati Dunia nzima mafuta yakiwa yamepanda Brazili Petroli inauzwa kwa bei ya chini na sababu kubwa ni wenzetu waliongeza uzalishaji kwenye Ethanol” Ameongeza Balozi Prof. Kilangi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *