
Kamati ya Kudumu ya Bunge Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC),imesema imeridhishwa na utendaji kazi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),na kutoa maelekezo yenye kuongeza ufanisi wa kukuza shirika hilo.
hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Jerry Silaa mapema leo Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada uwasilishwaji wa mipango mikakati na utekelezaji ambapo amesema shirika hilo limetekeleza kwa asilimia 100 kufuatia maelekezo waliyoyatoa mwaka jana.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NHC Nehemia Mchechu ametanabaisha uwepo wa mikakati wa Shirika hilo ikiwa ni pamoja na kufufua miradi iliyokuwa imesimama kwa muda mrefu na kujenga nyumba 5000 za kuuza na kununua hapa nchini kwa gharama ya Shilingi Bilioni 466 katika mradi wa Samia Housing Scheme (SHS) wanaotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.
