WAZIRI BASHUNGWA AINGIA MTAANI KUTETA NA WAFANYABIASHARA WADOGO

OR-TAMISEMI – Karagwe

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa leo ametembelea Wafanyabiashara wadogo na Wauza vyakula na kuteta nao kwenye maeneo tofauti ya Mji wa Kayanga, Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.

Katika matembezi hayo, Waziri Bashungwa amesikiliza mapendekezo na maoni yao juu hatua ambazo serikali inaendelea kuzichukua kwa kuboresha mazingira ya wafanyabiashara hao nchini.

Maeneo aliyotembelea Waziri Bashungwa ni pamoja na Soko la Wafanyabiashara wadogo eneo la Mabatini na wauza vyakula na wauza nguo za mitumba katika Mitaa tofauti ya Mji wa Kayanga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *