MAKAMU WA RAIS MSIBANI KWA MREMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango pamoja na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wamefika salasala
Jijini Dar es salaam nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour
Party (TLP) marehemu Augustine Lyatonga Mrema ili kutoa pole na kuifariji
familia, ndugu , jamaa na marafiki kufuatia kifo cha kiongozi huyo aliyefariki
tarehe 21 Agosti 2022 katika hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es salaam.
Akiwa nyumbani hapo, Makamu wa Rais amewapa pole wana familia na
kuwaomba kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu. Makamu wa
Rais amesema Marehemu Mrema alikuwa ni kiongozi mkweli na mzalendo kwa
taifa ambapo wakati wote alitetea maslahi ya nchi. Amesema taifa limepoteza
kiongozi aliyetumikia vizuri nafasi zote alizowahi kuongoza katika uhai wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *